Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAFANYA MKUTANO WA 'KLABU ZA TUSEME' SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI SHINYANGA

Shirika la Kimataifa la Save the Children kwa kushirikiana na shirika la Rafiki SDO la mjini Shinyanga wamefanya mkutano wa ‘Klabu z...


Shirika la Kimataifa la Save the Children kwa kushirikiana na shirika la Rafiki SDO la mjini Shinyanga wamefanya mkutano wa ‘Klabu za Tuseme’ kutoka shule 8 za msingi na sekondari katika manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya Shinyanga (Vijijini) kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya klabu hizo katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Disemba 6,2017 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha wanafunzi kutoka za shule za Ushirika, Mwasele,Solwa,Bugoyi A, Lyabusalu,Masekelo, Iselamagazi na Mwantini.
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children Alex Enock alisema klabu za Tuseme zimeundwa kupitia mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala unaotekelezwa na shirika la Save the Children kwa kushirikiana na Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la nchini Sweeden (SIDA).
Enock alisema lengo la klabu hizo ni kumsaidia mtoto wa kike kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kupewa ujauzito na kuepuka vishawishi mbalimbali ili aweze kumaliza masomo yake salama.
Naye afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement alisema katika kutekeleza mradi huo wameshirikiana na idara ya elimu msingi na sekondari kuanzisha klabu za Tuseme kwa ajili ya kuhamasisha ufaulu hasa kwa watoto wa kike.
“Wanafunzi katika klabu hizi tunawajengea uelewa juu ya masuala ya haki,wajibu na ulinzi wa mtoto pamoja kutoa mafunzo elekezi kwa viongozi na walimu walezi wa klabu hizi ili kupaza sauti kukataa ukatili dhidi ya watoto”,alisema Clement.
Wakizungumza katika mkutano huo,wanafunzi hao walisema klabu hizo zimewasaidia kwa kiasi kikubwa kujiamini,kuepuka vishawishi mbalimbali lakini pia wamekuwa mabalozi wazuri katika kuielemisha jamii juu ya haki za watoto.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika mkutano huo
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza wakati wa mkutano wa klabu za tuseme katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga leo- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza ukumbini
Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akizungumza katika mkutano huo wa klabu za tuseme
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ushirika akielezea namna klabu za tuseme zinavyosaidia katika kupigania haki za watoto.
Mmoja wa wanafunzi hao akielezea kazi za klabu za tuseme.
Wanafunzi wakielezea kuhusu klabu ya tuseme katika shule ya sekondari Mwantini.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A akielezea shughuli wanazofanya katika klabu yao ya tuseme
Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwasilisha mada kuhusu ukatili dhidi ya watoto
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiendelea kuwasilisha mada ukumbini
Walimu walezi wa wanafunzi klabu za tuseme wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakifanya kazi ya vikundi wakati wa mkutano huo
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi chao
Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi
Walimu walezi nao walikuwa na kazi kwenye kundi lao. Kulia ni Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwa katika kundi la walimu walezi wa wanafunzi
Washiriki katika mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAFANYA MKUTANO WA 'KLABU ZA TUSEME' SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI SHINYANGA
SAVE THE CHILDREN,RAFIKI SDO WAFANYA MKUTANO WA 'KLABU ZA TUSEME' SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI SHINYANGA
https://4.bp.blogspot.com/-DtpLv93Bmos/WigG781kjXI/AAAAAAAAVDE/-CTds5W9A9815olG9yS9PZ20utIUN6oiACLcBGAs/s640/UF3A0410.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-DtpLv93Bmos/WigG781kjXI/AAAAAAAAVDE/-CTds5W9A9815olG9yS9PZ20utIUN6oiACLcBGAs/s72-c/UF3A0410.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/12/save-childrenrafiki-sdo-wafanya-mkutano.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/12/save-childrenrafiki-sdo-wafanya-mkutano.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago