Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

RC GEITA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA LIPA KWA MATOKEO HALMASHAURI YA MJI GEITA.

Mhandisi Robert Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Mkoa na Wilaya Geita na kamati ya usalama ya Mkoa  wakikagua miun...


Mhandisi Robert Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Mkoa na Wilaya Geita na kamati ya usalama ya Mkoa  wakikagua miundombinu ya shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Halmashauri ya Mji Geita.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita(Wakwanza kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara yake katika Shule hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Geita akiingia ndani ya moja ya darasa lililojenjwa chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya Msingi Nguzo Mbili.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Mhandisi  Modest Apolinary  akifafanua jambo kuhusu utekelezaji miradi ya lipa kwa matokeo kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara yake shule ya msingi Nguzombili iliyopo Halmashauri ya Mji Geita.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Geita wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyotekelezwa kwa mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita.


Vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita.

                                                      (PICHA NA JUMAPILI MAGESA)


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo.  

" Inashangaza sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya Serikali"Alisema Lughumbi.

Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii.

Katika hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka  uongozi wa Shule ya Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa miundombinu hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka.  

 Aidha, ameagiza shule hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo vilivyojengwa vianze kutumika badala ya kufungwa.Pamoja na kutembelea Shule ya Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea shule ya Sekondari na kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo.

 Shule ya Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia shilingi milioni 13 kwa kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya kisasa pamoja na ukarabati wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na fedha iliyobaki katika bajeti ya darasa moja.

Mkoa wa Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali imeandaa mpango kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na jamii na wadau wote wa Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Imeandaliwa na mtandao wa maduka online.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: RC GEITA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA LIPA KWA MATOKEO HALMASHAURI YA MJI GEITA.
RC GEITA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA LIPA KWA MATOKEO HALMASHAURI YA MJI GEITA.
https://2.bp.blogspot.com/-IChwhemUTdE/WfsaC3uhKrI/AAAAAAAAdi8/lh02XPDYB98yW3_HyvYM0x-6CRI_hHriQCLcBGAs/s640/PICHA%2BNO.2.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-IChwhemUTdE/WfsaC3uhKrI/AAAAAAAAdi8/lh02XPDYB98yW3_HyvYM0x-6CRI_hHriQCLcBGAs/s72-c/PICHA%2BNO.2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/11/rc-geita-aridhishwa-na-utekelezaji-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/11/rc-geita-aridhishwa-na-utekelezaji-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago