Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TANESCO KUTUMIA WATALAMU WAKE KUJENGA VITUO NA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Lindi KATIKA kutekeleza dhana ya kujenga uzalendo na kubana matumizi, Shirika la Umeme Tanzania...
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Lindi
KATIKA kutekeleza dhana ya kujenga uzalendo na kubana matumizi, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia kampuni yake tanzu ya ETDCO, limeanza kutumia wataalamu wake wa ndani kujenga vutuo na njia za kusafirisha umeme.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, (Transmission), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(pichani juu), amesema kwa kuanzia, TANESCO ilitumia wahandisi na mafundi wake kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 132kv cha Mtwara na kingine cha Mahumbika Mkoani Lindi ikiwa ni pamoja na kujenga njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132Kv yenye urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mahumbika.
“Huu ni mwanzo mzuri kwetu tunaendelea kujenga vituo vingine na kituo kinachofuata kwenye mpango ni kile cha Kimbiji, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.” Alisema Mhandisi Bishaija wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea miundombinu ya TANESCO, kwenye mikoa ya Njombe, Songea, Mtwara na Lindi iliyofikia kilele Oktoba 16, 2017.
Akifafanua zaidi kuhusu azma hiyo ya Shirika, Mhandisi Bishaija alisema, miradi hiyo ya umeme ya Mtwara na Mahumbika, licha ya kukamilika ndani ya kipindi kifupi, lakini pia imekuwa ya ubora wa juu.
“TANESCO ilitumia uwezo (capacity) wa ndani kwa maana ya fedha, wahandisi na mafundi lakini pia hata jamii zinazozunguka vituo ndio walioshirikiana na mafundi wetu katika ujenzi wa vituo na njia hii ya kusafirisha umeme, na hakika mafanikio haya ndiyo yametupa ujasiri wa kuwa na mipango endelevu ya jkuendelea kutumia uwezo wetu sisi wenyewe.” Alisisitiza Mhandisi Bishaija.

Aidha Meneja wa TANESCO Mkoani Lindi Mhandisi Johnson Mwigune, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Mahumbika, umesaidia kuboresha hali ya umeme hii ni kutokana na urefu wa njia ya umeme kutoka Mtwara kuja Lindi, na kuwepo kwa michepuko mingi na transom nyingi, hitilafu ikitokea kwenye njia hiyo ilikuwa inasabisha mkoa mzima kukosa umeme, lakini sasa hivi matatizo ya katikati ya njia kati ya Mtwara na Lindi hayapo tena kutokana na uwepo wa kituo hiki.

 Kituo kipya cha kupoza umeme wa 132kV cha Mahumbika mkoani Lindi kilichojengwa na wahandisi na mafundi wa TANESCO mapema mwaka huu.

 Jengo la kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 132kV cha Mtwara kilichozindukliwa na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Machi 5, 2017.
 Meneja Mradi wa uboreshaji umeme mikoa wa Mtwara na Lindi, kutoka kampuni tanzu ya TANESCO, EDCO, Mhandisi Japhary Msuya, akielezea utekelezaji wa miradi hiyo.

 Transfoma mpya ya 132/32/Kv 30MVAkituo cha Mtwara.
Hapa ndipo umeme unapochukuliwa kutoka kituo cha Mtwara 132/33Kv kwenda kituo cha Mahumbika, 132/33kV mkoanin Lindi.
 Hii ndio kazi iliyofanywa na mafundi wazawa wa TANESCO
Hii ndio kazi iliyofanywa na mafundi wazawa wa TANESCO, ujenzi wa njia (line), ya 132kV kutoka Mtwara kwenda mkoani Lindi.
Mhandisi Bishaija, akizungumza na wahariri kwenye kituo cha kufua umeme utoknao na gesi cha, Mtwara.
 Meneja Mradi wa uboreshaji umeme mikoa wa Mtwara na Lindi, kutoka kampuni tanzu ya TANESCO, EDCO, Mhandisi Japhary Msuya, akiwaongoza wahariri kutembelea kituo cha Mtwara Oktoba 15, 2017.
Msimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtwara, akiwa kazini.
Gesi ikiunguzwa ili kuendesha mashine 8 za kufua umeme kituo cha umeme, Mtwara.
Gesi ikiunguzwa ili kuendesha mashine 8 za kufua umeme kituo cha umeme, Mtwara.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (kulia), akizungumza jambo na msimamizi wa mfumo wa udhibiti umeme kituo cha Mahumbika Bw.Juma Yahya Mshangama Oktoba 15, 2017. Wengine pichani ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Mhandisi Johnson Mwigune, na Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO Makao makuu, Bi. Leila Muhaji.Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Mhandisi Johnson Mwigune

<!--[if gte mso 9]>

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TANESCO KUTUMIA WATALAMU WAKE KUJENGA VITUO NA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME
TANESCO KUTUMIA WATALAMU WAKE KUJENGA VITUO NA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME
https://i.ytimg.com/vi/OOpS73KBW5A/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/OOpS73KBW5A/default.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/10/tanesco-kutumia-watalamu-wake-kujenga.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/10/tanesco-kutumia-watalamu-wake-kujenga.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago