Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS,SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES

Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan...


Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


Abraham Ntambara.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais.
Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine.
Aliahidi kuifanyia changamoto iliyotajwa ya matumizi ya mitandao ya kijamii ambapo alisema atalisimamia hilo kwani ni vizuri kutumia mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili kutokana na hivi sasa watu kuitumia vibaya.
Pia alitoa pendekezo la chama hicho kubuni miradi mingine ambayo inaweza kuwaingizia fedha ili kuacha kutegemea wahisani.

Mama Salma Kikwete wakati akimuachia jukumu hilo la kukilea chama hicho alimkabidhi vitu vitatu ambavyo ni Bendera ya Taifa ya chama, Katiba na mpango mkakati wa chama na kumvalisha Skafu ya chama kama ishara ya kukabidhiwa rasmi kijiti hicho.

Aidha alisema kuwa chama kimekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuweza kuongeza wanachama kutoka 97,143 hadi kufikia wanachama 100,008 mwaka huu.
Aliongeza kwamba wanatarajia mwezi Septemba kuapisha wanachama 300 katika mkoa huku akieleza kwamba tayari wamekwisha sajili zaidi ya wanachama 2000 katika mkoa wa lindi.

mwisho 
Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA


Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides


Samia akipata maelezo  kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA
Samia na Salma Kikwete wakilakiwa na Girl Guides
Brass Band ya Polisi ikiongoza wimbo wa Taifa
Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo
Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa
Kamishna Mkuu wa TGGA Symphorosa Hangi akisema neno la utangulizi pamoja na kutambulisha  wageni waalikwa 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo
Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia
Ni furaha iliyoje
Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan
Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo
Ni wakati wa furaha
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma

Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri
Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa  Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete
Mama Salma akionesha Saa hiyo


Girl Guides wakighani shairi maalumu
Baadhi ya makamishna wakiimba wimbo maalumu
NI FURAHA TELE
Viongozi na makamishna wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi mpya wa TGGA, Samia
Mlezi mpya, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na makamishna wa mikoa
Mama Samia na Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA
Girl Guides wakiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Mlezi mpya, Samia

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS,SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES
MAKAMU WA RAIS,SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES
https://1.bp.blogspot.com/-Rm9WUl6Ul5M/WWYhZfwktsI/AAAAAAABFyI/D6vup7_MaAca5BeXb9Ue3vvefPFFVo8AACLcBGAs/s640/IMG_9724.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-Rm9WUl6Ul5M/WWYhZfwktsI/AAAAAAABFyI/D6vup7_MaAca5BeXb9Ue3vvefPFFVo8AACLcBGAs/s72-c/IMG_9724.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/07/makamu-wa-raissamia-amrithi-mama-salma.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/07/makamu-wa-raissamia-amrithi-mama-salma.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago