Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

BANK OF AFRICA TANZANIA YAFUNGUA MATAWI MWANZA NA MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella akizindua rasmi tawi la Nyanza-Mwanza na lile la Uluguru-Morogoro Naibu Mkurugenzi mtendaji...


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella akizindua rasmi tawi la Nyanza-Mwanza na lile la Uluguru-Morogoro

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania Wasia Mushi akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Mwanza zawadi ya Visa Prepaid Card (TOUCAN CARD) ambayo itamwezesha mkuu huyo wa mkoa kufanya online purchases pamoja na kupata huduma za kifedha kwenye ATM machine Zaidi ya Milioni tatu zilizopo sehemu mbalimbali duniani.

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania Wasia Mushi akitoa hotuba katika uzinduzi wa matawi mawili ya Bank of Africa Tanzania Mwanza na Morogoro. Uzinduzi wa matawi haya unafanya benki hiyo kua na jumla ya matawi 27 nchi nzima.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba yake katika halfla ya uzinduzi rasmi wa matawi mawil ya Bank of Africa Tanzania.


Akizungumza mkoani Mwanza, wakati akizindua matawi mawili kwa pamoja ya Bank of Africa Tanzania tawi la Nyanza lililopo jijini Mwanza na wakati huo huo tawi la Uluguru lililopo jijini Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella alisema ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki na kwamba Mwanza ni ya pili kuchangia katika pato la taifa.

“Nimesikia kwamba mna matawi 27, huu ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki. Naomba mfahamu kwamba Mwanza inachangia asilimia 7 ya pato la taifa. Bank of Africa Tanzania natambua kuwa mnasaidia juhudi za serikali kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi,”alisema Mh. Mongella.

Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa matawi hayo kwa pamoja, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi alisema : “Benki ya Afrika ipo katika nchi 18 na kwamba makao yake makuu yapo Dakar, Senegal. Hapa nchini ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam na jumla ya matawi 27.”

Mushi alisema katika kipindi cha miaka 10 benki hiyo imekuwa benki muhimu, imara endelevu kwa kutoa huduma zake za kibenki kwa watu mbalimbali wakiwamo wateja wakubwa, wadogo na wa kati.

“Mwanza inajulikana zaidi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uvuvi katika Ziwa Victoria, uchimbaji wa madini, kilimo cha pamba na utoaji wa huduma katika sekta mbalibali, hivyo ni muhimu wakatumia huduma za Bank of Africa Tanzania,”alisema.

Alisema benki hiyo imedhamiria kuleta mapinduzi kwenye sekta za kibenki kwa kutoa huduma stahiki ambazo zitaweza kumfikia kila Mtanzania kwa njia nyepesi kupitia wafanyakazi wao.

“Tawi la Nyanza na tawi la Uluguru yote yamefunguliwa kwa pamoja, hii ni benki ya biashara ambayo imeanzishwa mwaka 2007. Leo ina matawi 27 katika maeneo mbalimbali nchini”

Alisema kwa sasa benki hiyo inatoa mikopo mbalimbali ikiwamo ya ukarabati wa nyumba, kutumia nyumba kama dhamana ya kupata mitaji ya biashara au kusaidia kujenga nyumba nyingine.

“Kwa pamoja Bank of Africa Tanzania imeungana na shirika la maendeleo la Ufaransa AFD kwa manufaa ya kuwezesha watu mbalimbali wanao jikita kwenye shughuli za nishati endelevu na mbadala,”alisema Mushi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: BANK OF AFRICA TANZANIA YAFUNGUA MATAWI MWANZA NA MOROGORO
BANK OF AFRICA TANZANIA YAFUNGUA MATAWI MWANZA NA MOROGORO
https://4.bp.blogspot.com/-JBityykL_LI/WKCkSvNsA4I/AAAAAAAAFcA/EcJ45adVlfoJ_6gPRafA0-ftUxe8EiEBQCLcB/s640/3.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-JBityykL_LI/WKCkSvNsA4I/AAAAAAAAFcA/EcJ45adVlfoJ_6gPRafA0-ftUxe8EiEBQCLcB/s72-c/3.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/02/bank-of-africa-tanzania-yafungua-matawi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/02/bank-of-africa-tanzania-yafungua-matawi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago