Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE, YASEMA GRIDI YA TAIFA IKO SALAMA

Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(katikati), akionyesha kifaa kilicholipi...Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(katikati), akionyesha kifaa kilicholipika (female connector), cha umeme wa 132kv kutoka Ubungo kwenda Chalinze. Kulia ni KaimunMeneja Uhusiano, Bi. Leila Muhaji na kushoto ni mwangalkizi mkuu wa kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, Bw,Deodatus Ngwanda

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeeleza chanzo cha kukatika umeme leo Januari 25, 2017), ni kulipuka kwa kikata umeme,(Circuit breaker), baada ya kifaa kijulikanacho kama female connector ya umeme wa 132kv kutoka kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda Chalinze mkoani Pwani kupata hitilafu.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(pichani juu), alisema hitilafu hiyo iliyotokea majira ya saa 12;32 asubuhi, leo Januari 25, 2017  ilileta athari kwenye mfumo mzima wa gridi ya taifa na kufanya wateja wa TANESCO walio kwenye mikoa inayotumia gridi ya taifa kukosa umeme kwa takriban masaa mawili.
"Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa gridi ya taifa iko salama, hakuna tatizo lolote isipokuwa ilizima baada ya kikata umeme hicho kulipuka, lakini sasa mambo yamewekwa sawa na umeme unazidi kurejea katika hali yake ya kawaida kote nchini" alisema Mhandisi Issa, wakati waandishi wa habari walipopelekwa kujionea wenyewe hitilafu hiyo majira ya mchana leo. Hata hivyo alisema kifaa kilichoharibika kinasafirishwa kutoka mkoani Tanga, na mara kitakapowasili kitafungwa mahala kilipoharibika kile cha awali.
 Hii ndiyo kikata umeme (Circuit breaker) iliyolipuka
 Female Connector inayotoa umeme hapo ubunge kupeleka Chalinze mkoani Pwani ambayo ililipuka
 Female connector (juu katikati) iliyolipuka
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi Leila Muhaji, akiwa na baadhi ya waandshi wa habari waliotembelea eneo hilo leo mchana Januari 25, 2017
COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE, YASEMA GRIDI YA TAIFA IKO SALAMA
TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE, YASEMA GRIDI YA TAIFA IKO SALAMA
https://1.bp.blogspot.com/-WZh-WTwwRPs/WIifN4p5oXI/AAAAAAAAxcg/ZaZwMuYgyyQ4cF9ZePUuOOM24Z_o-CMBACLcB/s640/SOURCE.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-WZh-WTwwRPs/WIifN4p5oXI/AAAAAAAAxcg/ZaZwMuYgyyQ4cF9ZePUuOOM24Z_o-CMBACLcB/s72-c/SOURCE.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2017/01/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wake-yasema.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2017/01/tanesco-yawatoa-hofu-wateja-wake-yasema.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago