Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KINANA AONGOZA MAZISHI YA MUASISI WA TANU KHADIJA KAMBA

Na Bashir Nkoromo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza mamia ya wananchi katika maziko ya muasisi wa chama cha Tanganyik...Na Bashir Nkoromo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza mamia ya wananchi katika maziko ya muasisi wa chama cha Tanganyika African Union (TANU) na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khadija Kamba, aliyefariki jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kinana ambaye alifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akitoa salam za rambirambi za Chama, alisema, CCM itamkumbuka na kuuenzi daima mchango mkubwa alioutoa hasa wakati wa harakati za ujenzi wa TANU na harakati za ukombozi wa Tanzania wakati wa uhai wake.

"Binti Kamba alikuwa ni nguzo na chachu muhimu katika kuasisiwa kwa TANU na mpambanaji aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutafuta Uhuru wa nchi hii, hivyo Chama kitambukumbuka na kumuenzi daima Mama huyu", alisema Kinana, wakati akitoa salam za rambirambi wakati wa maziko.

Kinana alisema, licha ya kuwa muasisi, lakini Binti Kamba kamtika maisha yake, aliendelea kuwa nwanachama na kada mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi na kuendelea kuwa kisima cha kuchota hekima na maarifa hadi anafariki dunia.

Alisema, kutokana na kuguswa na msiba huo, kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu wa Chama, ameandaa hitima itakayosomwa keshokutwa katika Msikiti wa Masjid Quba, kumuombea maghfira.

Binti Kamba, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 94, alifariki jana asubuhi, nyumbani kwa mwanae wa kulea, Kamba Abdallah, jijini Dar es Salaam, kutokana na kuugua figo na moyo.

Msafara kwenda kwenye maziko Kisutu ulianzia nyumbani kwa marehemu, Ilala Bungoni, Dar es Salaam, baada ya kuswaliwa, ambako miongoni mwa waombolezaji waliokuwepo ni pamoja na Muasisi mwingine wa TANU Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye mwaka jana alihamia Chadema kumfuata aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Edward Lowassa. PICHA NYINGI ZA MAZISHI HAYO/>>BOFYA HAPA

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KINANA AONGOZA MAZISHI YA MUASISI WA TANU KHADIJA KAMBA
KINANA AONGOZA MAZISHI YA MUASISI WA TANU KHADIJA KAMBA
https://3.bp.blogspot.com/-JChGULYdsiU/WEAx5UlCBEI/AAAAAAABVeI/eWr7C3naLDEQivCe0HlvvY8TMMKnMj00gCLcB/s640/1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-JChGULYdsiU/WEAx5UlCBEI/AAAAAAABVeI/eWr7C3naLDEQivCe0HlvvY8TMMKnMj00gCLcB/s72-c/1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/12/kinana-aongoza-mazishi-ya-muasisi-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/12/kinana-aongoza-mazishi-ya-muasisi-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago