Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WASANII WA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU.o

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wasanii wa Filamu mkoani Geita hii ...


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wasanii wa Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.

Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa pili kushoto).

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Na BMG
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Geita waliohudhuria kikao baina yao na Bodi ya Filamu mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso, ambapo amewasisitiza kuungana pamoja na kutengeneza filamu moja iliyo bora kwa ajili ya kuwatambulisha kwenye soko la filamu na pia kuutambulisha mkoa wa Geita badala ya kuwa na filamu nyingi zisizo na ubora.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye.

Wanaofuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fessoo, Mwakilishi wa balozi wa Tanzania nchini Denmark, Dotto Kahindi pamoja na Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Robert Manondolo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wasanii wa Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akisisitiza wasanii mkoani Geita kushikamana na kushirikiana na viongozi wao pamoja na Serikali na kuandaa Maonesho ya sanaa kwa kuwa fursa hiyo wanayo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wasanii wa Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye,
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita amesema viongozi wa serikali mkoani Geita wakiwemo Maafisa Utamaduni wako tayari kutoa ushirikiano wao ili kuboresha sanaa mkoani humo.

Amewapa chachu wasanii wa Filamu mkoani Geita kuungana pamoja na kutengeneza kazi bora kwani sanaa hiyo inaweza kubadilisha maisha yao na kuwa mabilionea ikiwa watafanya kazi bora.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael, amebainisha kwamba chama hicho kimeweka mikakati ya kuboresha soko la filamu mkoani Geita huku matamanio yao ni kuwa na Maonesho ya sanaa yatakayotoa fursa kwa wasanii kuonesha kazi zao.
Mmoja wa wasanii wa filamu mkoani Geita akisoma risala kwa niaba ya wasanii wengine ambapo amebainisha kwamba wanasanii wa filamu mkoani Geita wanahitaji kupewa mafunzo zaidi namna ya kuboresha kazi zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi zao hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao.
Wasanii mkoani Geita wanasema bado hawanufaiki na uuzaji wa kazi zao kwa kuwa zinaoneshwa bure kwenye baadhi ya visimbuzi nchini pamoja na kudurufiwa (kunakiliwa) kwa wingi mitaani hivyo bodi ya filamu iwasaidie namna ya kuzisajili ili kulinda maslahi yao.
Wasanii wa filamu mkoani Geita wameshauri kiundwe kikosi kazi kwa ajili ya kukomesha udurufishaji (kunakiliwa) wa kazi zao mitaani kwa kuwa zinasababisha kukosa stahiki zao.
Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wameomba mazingira ya ukaguzi wa filamu yaboreshwe zaidi ili kuwapa fursa ya filamu zao kukaguliwa.
Waigizaji, waongozaji wa filamu na watunzi wa hadithi za filamu na tamthilia ni miongoni mwa makundi yanayokamilisha sanaa ya filamu.
Kikao baina ya Wasanii wa Filamu/Tamthilia mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.
Picha ya pamoja katika viongozi mbalimbali akiwemo mgeni rasmi Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa nne kulia) na wasanii wa filamu mkoani Geita
Na George Binagi-GB Pazzo
Wasanii wa Filamu mkoani Geita wamepewa mtihami ambao hata hivyo ni mwepesi ikiwa watakuwa na dhamira ya dhati ya kuikuza tasnia hiyo. 

Mtihani huo umetolewa hii leo na Waziri wa Afya Zanziar, Mahmood Kombo, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye kikao baina ya wasanii wa filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.

Mtihani wenyewe ni wasanii hao kuandaa Tamasha la Filamu mkoani Geita ambalo litasaidia kuinua tasnia hiyo mkoani humo, Kanda ya Ziwa na hata nchini kwa ujumla.

"Mkitayarisha Tamasha lenu, mimi mwakani nitakuja pamoja na familia yangu". Amesisitiza Waziri Kombo akitolea mfano Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar namna linavyofana na kuwatangaza wasanii pamoja na kuwaongezea kipato.

Hata hivyo wasanii wa filamu mkoani Geita kwenye risala yao wamesema wanahitaji kupewa mafunzo zaidi juu ya namna ya kuboresha filamu zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi hizo hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao na kuahidi kufikisha mafunzo ya filamu mkoani Geita kama ilivyokuwa hivi karibuni mkoani Mwanza.

Tazama HAPA Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WASANII WA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU.o
WASANII WA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU.o
https://4.bp.blogspot.com/-DA5MZpf44Ow/WDAtaW2PFBI/AAAAAAAAPVY/DsR5za00ebIye2Ryym6acnBxlsm4knmVwCLcB/s640/1.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-DA5MZpf44Ow/WDAtaW2PFBI/AAAAAAAAPVY/DsR5za00ebIye2Ryym6acnBxlsm4knmVwCLcB/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/11/wasanii-wa-filamu-mkoani-geita-wapewa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/11/wasanii-wa-filamu-mkoani-geita-wapewa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago