Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo w...
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali kabla hajahutubia hotuba yake ya  ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
 Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
 Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.

Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara  baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
                                   .......................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo haki ya kuishi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati anafungua mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.

 Amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza ipasavyo mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya na elimu bila kubaguliwa kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya Dunia yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo haki ya kuishi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki sawa katika jamii.Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuingiza wanawake katika ngazi za maamuzi na kwa sasa mpango kabambe unafanyiwa kazi ili kuhakikisha sekta binafsi ambayo bado inaidadi ndogo ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kufanya hivyo na kwamba tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini zinaonyesha kuwa wanawake wengi walioingizwa kwenye bodi mbalimbali bodi hizo kwa sasa zimeongeza ufanisi wa kazi maradufu.

Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Justice Sylvain Ore amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kujadili na kuweka mikakati inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika zinazingatia na kulinda haki za bindamu hasa haki za wanawake kwa kiwango kikubwa.

Mkutano huo wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ambao unafanyika Jijini  Arusha umehudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Afrika AU na lengo la mkutano huo  ni kutajadili masuala ya demokrasia na haki za binadamu katika nchi za Afrika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA
https://1.bp.blogspot.com/-IzhW1j2fGx4/WDV8Pj0d25I/AAAAAAAAzmw/fyeL6jjzj1g3FEEd_4z22KAf5guVc-aUACEw/s640/2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-IzhW1j2fGx4/WDV8Pj0d25I/AAAAAAAAzmw/fyeL6jjzj1g3FEEd_4z22KAf5guVc-aUACEw/s72-c/2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/11/makamu-wa-rais-mhe-samia-afungua.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/11/makamu-wa-rais-mhe-samia-afungua.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago