Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI

KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI Na Mwandishi Wetu, Mbeya. Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Wilaya y...


KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI


Na Mwandishi Wetu, Mbeya.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Wilaya ya Mbeya mjini, kimeingia kwenye mgogoro baina ya viongozi  na madiwani.

Mgogoro huo, ambao unatajwa  kujikita zaidi kwenye maslahi binafsi ya watu, huenda ukakiathiri chama hicho kwa kutengeneza mpasuko, kama uongozi wa juu hautachukua hatua za haraka.

Chanzo cha mgogoro huo,unadaiwa umetokana na viongozi wa chama hicho kujaribu kutengeneza mazingira ya kuwafuta uanachama baadhi ya madiwani kutokana na mienendo ya utendaji kazi wao kutoridhisha.Inatajwa kuwa chama hicho, hakikuridhishwa na utendaji kazi wa madiwani hao hivyo kuwaandikia barua  yenye kumbu kumbu namba CDM/MBY/11/2016/41 iliyosainiwa na Kaimu Katibu Raphael Mwaitege inayowataka  kuhudhuria mkutano mkuu wa wilaya mbeya mjini.Pia,Madiwani  wote wametakiwa kutoa  maelezo ni kwa nini hawakuudhulia kikao kilichopita cha tarehe 28/9/2016, kushindwa kushiriki shughuli za kijamii kama vile misiba, kutaja idadi ya vikao vya baraza walivyoshiriki pamoja michango ya kifedha waliyokichangia  chama.Mratibu wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini(CHADEMA), Franky Mwaisumbe, amesema ofisi baada ya kupokea taarifa hiyo iliunda tume ili kufanya uchunguzi wa madai hayo na kwamba imeanza kufanya kazi  November 14, mwaka huu.Kazi kubwa itakayofanywa na tume hiyo ni  kuwaita na kuwahoji madiwani wanaotuhumiwa, kuwahoji wananchi juu ya utendaji kazi wa madiwani wao.Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Obadia Mwaipalu alipohojiwa kuhusu mkanganyiko huo, alikana taarifa za chadema Wilaya kuwaandikia madiwani hao barua kwa lengo la kutaka kuwahoji na kwamba hakuna mgogoro ndani ya chama hicho.Huku hayo yakiendelea kwa upande wa uongozi, baadhi ya madiwani  wameeleza kusikitishwa na hatua za viongozi wa chama ngazi ya Wilaya kujikita katika kutengeneza migogoro ndani ya chama badala ya kuwapa woa nafasi ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waliofanikisha kuiweka chadema madarakani na kushika halmashauri.Wamesema, ni mambo mengi yamekuwa yakifanywa na uongozi wa juu wa Wilaya ambayo yamekuwa hayana ustawi mzuri kwa ndani ya chama.“Kunaviongozi wamefika mahala, wamekuwa wakidiriki hata kuwatukana kwa kuwarushia matusi ya nguoni madiwani viti maalum  na ukiuliza sababu huioni, ukiacha hilo viongozi hao wamekuwa wakiwashawishi wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya maandamano wakitaka Meya ajiuzulu kutokana na kushindwa kushughulikia posho zao,”kilisema chanzo cha habari hii.Sasa ukiangalia posho za wenyeviti zinahusisana nini na meya…. kwani licha ya suala lao kushughulikiwa na mkurugenzi wa halmashauri lakini bado viongozi hao wameendelea kutengeneza malumbano yasiyokuwa na tija.Tunafahamu kinachotakiwa hapa ni nafasi ya Umeya na si kingine  lakini ni vema taratibu zikafuatwa kuliko kutengeneza skendo zisizokuwa na maslahi kwa chama na kwa wananchi kwa ujumla.(JamiiMojaBlog)Mwisho.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI
KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI
https://3.bp.blogspot.com/-jID7qawhjz8/WCxujRb_PfI/AAAAAAAAWyU/lyPJgs0-ueUJClghV_zwCTajXkm3IzTSwCLcB/s320/meya.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-jID7qawhjz8/WCxujRb_PfI/AAAAAAAAWyU/lyPJgs0-ueUJClghV_zwCTajXkm3IzTSwCLcB/s72-c/meya.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/11/kiti-cha-umeya-chaivuruga-chadema-mbeya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/11/kiti-cha-umeya-chaivuruga-chadema-mbeya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago