Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

ESRF YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA UTAFITI

Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imezindua MPANGO Mkakati wa miaka mitano 2016 – 2020 ambao umeainisha vipaumbele saba kw...


Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imezindua MPANGO Mkakati wa miaka mitano 2016 – 2020 ambao umeainisha vipaumbele saba kwa kufanyia Utafiti katika masuala mbalimbali ya Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shabani kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James.

Mpango Mkakati huo 2016 – 2020 ambao ni wa sita tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo,umeainisha maeneo makuu saba ambayo ndani ya maeneo hayo kuna maeneo mengine madogo madogo ishirini na sita ambayo kwa pamoja yatatiliwa mkazo katika kipindi hicho cha miaka mitano.

Maeneo hayo makuu ni; Kukuza Uchumi, Ajira na Viwanda; Utawala na Uwajibikaji; Utandawazi na Ushirikiano wa kikanda; Utoaji wa huduma na ulinzi wa kijamii; Mali asili na Usimamizi wa Mazingira; Usimamizi wa Maarifa na Ubunifu pamoja na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (wa pili kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za ESRF kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF kuzindua Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020. Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kushoto) pamoja na Mshehereshaji wa uzinduzi wa mpango mkakati huo, Prof. Samuel Wangwe (wa pili kushoto).(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Bi. Amina alisema kwamba serikali imefurahishwa sana na juhudi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)

kusaidia serikali kusukuma mbele huduma zake kwa jamii na kupanua uwezo wa kutengeneza Taifa linalotekeleza sera za ukuaji wa uchumi.

Aliwapongeza waandaaji wa Mpango Mkakati huo na kusema Wizara yaFedha na Mipango inafurahishwa sana na namna Taasisi hiyo kama chombo cha Utafiti kinavyosaidia kuonyesha njia na kutoa mwelekeo kwa masuala mbalimbali ya kisera na utekelezaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na Mpango Mkakati huo, serikali imefurahishwa kuona kuwa taasisi hiyo pia imejikita katika kusaidia kuona serikali inafanikisha utekelezaji wa maendeleo endelevu nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akizungumza kabla ya kumkarisbisha mgeni rasmi Bi. Amina kuzindua Mpango Mkakati huo pamoja na mambo mengine alisema kwamba Taasisi yake imejikita katika kufanya tafiti maeneo saba ambayo yamo katika mpango wa pili wa maendeleo.

Wadau katika kujadili Mkakati huo wameiomba Serikali kufanikisha Tafiti zote zilizokusudiwa kufanywa zinatekelezwa kwa kuisaidia Taasisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida akizungumza machache na kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James kwenye uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika hafla ya uzinduzi huo.
Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswald Mashindano akielezea wadau mbalimbali mambo muhimu yaliyomo katika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akikata utepe kuzindua rasmi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) kwa pamoja wakiwa wameshika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 wakipitia mpango mkakati huo uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Sehemu ya wadau, wageni waalikwa na wafanyakazi wa ESRF katika hafla hiyo ya uzinduzi.


Pichani juu na chini ni wageni waalikwa walioshiriki kwenye uzinduzi huo wakitoa maoni juu ya mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.
MC ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya ufundi inayotoa ushauri kwa menejimenti ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF, jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: ESRF YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA UTAFITI
ESRF YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA UTAFITI
https://images-blogger-opensocial.googleusercontent.com/gadgets/proxy?url=http%3A%2F%2Fdewjiblog.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2016%2F11%2FIMG_8446.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/11/esrf-yazindua-mpango-mkakati-wa-miaka.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/11/esrf-yazindua-mpango-mkakati-wa-miaka.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago