Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

CHUO KIKUU IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA .....

                                                             Rais Dkt John Magufuli   Wahitimu   Aziza Mkawa na Amina Ally  waki...

 Image result for Rais Magufuli
                                                           Rais Dkt John Magufuli 


 Wahitimu   Aziza Mkawa na Amina Ally  wakimlisha  keki  mwenzao Eugenia Msahala aliyehitimu jana  chuo  kikuu  cha Iringa

Wahitimu  wa chuo  kikuu cha Iringa  Rubeny Nyagawa kulia ,Anna Laiza , Deodatus Mnyang'ari na Anna Lwanda wakijipongeza kwa  keki baada ya  kuhitimu digirii  ya  biashara  na utawala katika  chuo  kikuu cha Iringa
-----
 Na MatukiodaimaBlog
UONGOZI  wa  Chuo kikuu cha Iringa (UoI) umepongeza   jitihada  zinazofanywa na  serikali ya  awamu ya  tano  chini  ya Rais  Dkt John  Magufuli juu ya uhakiki wa   watumishi  hewa wenye  vyeti  feki kwa madai  hatua   hiyo  ni  nzuri  itasaidia kupata  wataalam wenye  sifa sahihi   tofauti na  ilivyokuwa  awali kuwa na utitiri  wa   watumishi  wasio na uwezo.


Pongezi  hizo  zimetolewa jana   wakati wa  mahafali ya chuo  hicho na mwenyekiti wa Bodi ya Chuo,  askafu  wa kanisa la  kiinjili  la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya  Iringa  Dkt. Odenburg  Mdegela alisema kuwa zoezi hilo linapembua mchele na chuya na kuwaacha wale wenye vyeti halai tu.

Alisema ilikuwa si sahihi mmoja akae darasani miaka mitatu na mwingine apate cheti kutoka kariakoo tena kikiwa a ufaulu wa juu kuliko Yule aliyekaa darasani.


Dkt. Mdegela alisema watu hawa wanapokutana kazini Yule alipata vyeti bandia vyenye ufaulu wa hali ya juu anakuwa hajui kazi jambo lililokuwa likirudisha nyuma maendeleo ya taasisi nyingi na nchi kwa ujumla.


“Uhakiki wa vyeti unapaswa kuungwa mkono na wadau wote wakiwemo wa elimu kwa kuwa hali ilikuwa mbaya huku wale wenye vyeti badia vikiwa na ufaulu wa hali ya juu ilhali hawajui kazi”, alisema Dkt. Mdegela


Aidha alisema Chuo hicho kinajipanga kuachana na mtazamo uliojengeka kwa muda mrefu wa kujiendesha kwa kutegemea wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya nchi pamoja na mikopo ya ada za wanafunzi kutoka serikalini.


Alisema wanatarajia kuanzisha Asasi itakayokuwa imeungwanishwa na Chuo ambayp itakuwa ikitoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi ambao wamekwama kupata huduma hiyo kutoka maeneo mengine.Kwa  upande  wake mkuu wa Chuo hicho, Jaji mkuu mstaafu Augustine Ramadhani alisema ni vema wahitimu wakawa wazalendo kwa nchi yao na kuitumia elimu waliyoipata kwa maendeleo ya watanzania wote.


Huku makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Joseph Madumula alisema mazingira ya utoaji wa elimu kwa sasa yamekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na Chuo kikuu kimoja cha Dar es Salaam kikiwa na matawi mawili ya Sokoine na Muhimbili.


Aliongeza kuwa kwa sasa kuna zaidi ya vyuo vikuu 60 vya binafsi na serikali lakini idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa haijaongezeka kulingana na vyuo idadi ya vyuo.

Alisema wamejipanga kutoa elimu shirikishi ya ujasiliamali kwa wanafunzi wote wa Chuo hicho ili wakimaliza wasitegemee kuajiriwa tu bali wawe na uwezo wa kujiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana wengine.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: CHUO KIKUU IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA .....
CHUO KIKUU IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA .....
http://www.eatv.tv/sites/default/files/news/2016/09/20/magufuli%20pasport.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-wdtgmjHd_ks/WDGADHB0kyI/AAAAAAACN-8/ez7zqNJDPmQJS44oiC0pLpikwWu5d-4PQCLcB/s72-c/DSC_0089.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/11/chuo-kikuu-iringa-wampongeza-rais-dkt.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/11/chuo-kikuu-iringa-wampongeza-rais-dkt.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago