Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MCHANGO WA UINGEREZA WAENDELEZA UTOAJI MISAADA KWA WAKIMBIZI NCHINI

Wakimbizi wakigaiwa msaada wa chakula kwenye kambi zao. (Picha zote na Tala Loubieh wa WFP). Ni kutokana na mchango mkubwa wa Paun...


Wakimbizi wakigaiwa msaada wa chakula kwenye kambi zao. (Picha zote na Tala Loubieh wa WFP).

Ni kutokana na mchango mkubwa wa Paundi za Uingereza milioni 1 (Dola za Marekani milioni 1.3) kutoka katika Shirika la Misaada la Uingereza (Department for International Development --DFID), kwamba Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeweza, walau kwa muda, kusitisha mpango wa kupunguza kiasi cha mgao wa chakula uliopangwa kwa ajili ya wakimbizi nchini Tanzania.
 Wakimbizi wakigaiwa msaada wa chakula kwenye kambi zao. (Picha zote na Tala Loubieh wa WFP).
WFP ilikuwa imepanga kupunguza kiasi cha mgao kuanzia Oktoba kwa karibu robo milioni ya wakimbizi kutokana na kukosekana kwa fedha za kuendeshea shughuli za WFP za kuhudumia wakimbizi nchini Tanzania. Sasa – walau kwa muda huu – shughuli hizi zitaendelea kama kawaida.
“Uingereza inaungana na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa katika kusaidia ukarimu mkubwa wa Serikali na watu wa Tanzania wa kuwakaribisha wale wanaotafuta usalama kutokana na mapigano nchini Burundi na ukanda wa Maziwa Makuu,” alisema Vel Gnanendran, ambaye ni Mkuu wa DFID. “Kwa hiyo, tunatoa mchango wa nyongeza mara moja wenye thamani ya Paundi milioni 1 ili kuisaidia WFP kuendelea kutoa chakula kwa idadi inayokuwa ya wakimbizi wanaowasili nchini Tanzania. Nyongeza hii inafanya jumla ya mchango wetu kwa WFP kufikia Paundi milioni 6.5 tangu mgogoro huu uanze.”

WFP husambaza chakula kinachookoa maisha kwa wakimbizi wapatao 236,000 wanaoishi katika kambi tatu mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania. Wakimbizi wanategemea msaada huu, ambao ni pamoja na mahindi, kunde, mafuta ya kupikia, chumvi na mchanganyiko wa uji wenye virutubisho.

“WFP inatoa shukrani za dhati kwa DFID kwa mchango wao katika kipindi hiki muhimu,” alisema Michael Dunford, Mwakilishi wa Nchi wa WFP nchini Tanzania. “Wakati ambapo fedha zaidi za nyongeza zinahitajika haraka ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hadi kufikia mwisho wa mwaka huu, tunathamini sana mchango huu mkubwa.”

Licha ya kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kikalori ya kila siku ya wakimbizi, WFP hutoa chakula kilichopikwa katika vituo vya mpito na kupokelea wakimbizi na vituo vya afya. Katika kambi za wakimbizi, WFP pia husaidia akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha, na pia watoto wenye utapiamlo wa kiwango cha kati walio na umri wa chini ya miaka mitano kwa kuwapatia unga wenye virutubisho au mchanganyiko wa uji ulioongezewa virutubisho.

Kila siku, mamia ya wakimbizi kutoka Burundi huwasili katika mpaka wa Tanzania, hasa kutokana na kuendelea kwa mapigano nchini mwao. WFP inamudu kutimiza wajibu wake kutokana na misaada itokayo kwa wahisani. Lakini kutokana na kuendelea kumiminika kwa wakimbizi, Shirika lina hali ngumu ya kifedha. Michango isipoongezeka, usalama wa chakula na lishe wa wakimbizi unaweza kuwa katika hatari kubwa.

Ili kuendeleza shughuli za kuwahudumia wakimbizi hadi mwisho wa mwaka, WFP inahitaji Dola za Marekani milioni 7.6. Jumla ya Dola za Marekani milioni 63.6 zinahitajika hadi kufika Agosti, 2017.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MCHANGO WA UINGEREZA WAENDELEZA UTOAJI MISAADA KWA WAKIMBIZI NCHINI
MCHANGO WA UINGEREZA WAENDELEZA UTOAJI MISAADA KWA WAKIMBIZI NCHINI
https://2.bp.blogspot.com/-BkEZI18rI5U/V_YaGwiaKhI/AAAAAAABnOk/cAwzY9zGVjcMukxOot5J8SVGpZv6hkEEQCLcB/s640/Copyright-WFP-Tala-Loubieh-3.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-BkEZI18rI5U/V_YaGwiaKhI/AAAAAAABnOk/cAwzY9zGVjcMukxOot5J8SVGpZv6hkEEQCLcB/s72-c/Copyright-WFP-Tala-Loubieh-3.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/10/mchango-wa-uingereza-waendeleza-utoaji.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/10/mchango-wa-uingereza-waendeleza-utoaji.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago