Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI FINLAND

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland...


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto) masuala mbali mbali ya uwekezaji,elimu na uwezeshaji Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
                          ............................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem

Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.


Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.

Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote nchini.


Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.
Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI FINLAND
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI FINLAND
https://2.bp.blogspot.com/-zHkWu4UV43E/WBMVH_l78zI/AAAAAAAAzU4/boI40NvfECciXnUCfxaFgLf4BSmhwVT2QCLcB/s640/3.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-zHkWu4UV43E/WBMVH_l78zI/AAAAAAAAzU4/boI40NvfECciXnUCfxaFgLf4BSmhwVT2QCLcB/s72-c/3.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/10/makamu-wa-rais-mhe-samia-akutana-na.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/10/makamu-wa-rais-mhe-samia-akutana-na.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago