Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

LHRC YAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI KUPINGA ADHABU YA KIFO

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (katikati),  Mkurugenzi wa Uwezeshaji na...


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (katikati), Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia) na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga , wakionesha jarida la kupinga adhabu ya kifo wakati wa uzindi wake Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.
 Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na mauaji.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali  wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.

Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo  kwa sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku  wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.

Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo  Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi  mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Alisema kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na ugaidi.

Dk. Bisimba alisema kituo  kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya kifo na  hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata muuaji auawe.

“Adhabu ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu  kwa wale watu ambao huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk. Bisimba na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza kuzuia watu wengine kutokutenda makosa  kama hayo.

Alisema licha ya adhabu  hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban miaka 22 , taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa kutokana na adhabu hiyo.

Hata hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii juu ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira ya kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria  kwa kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vya muda mrefu  gerezani.COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: LHRC YAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI KUPINGA ADHABU YA KIFO
LHRC YAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI KUPINGA ADHABU YA KIFO
https://4.bp.blogspot.com/-hswUZnOtU%0A8A/V_uNrD6sAmI/AAAAAAAAYHo/XkbohyT2OawZj8eQqIcvGxG_U2CV_E2-ACLcB/s640/1.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-hswUZnOtU%0A8A/V_uNrD6sAmI/AAAAAAAAYHo/XkbohyT2OawZj8eQqIcvGxG_U2CV_E2-ACLcB/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/10/lhrc-yafungua-kesi-dhidi-ya-serikali.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/10/lhrc-yafungua-kesi-dhidi-ya-serikali.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago