Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watete...Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.

Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli za utetezi.

Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010 ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe ruzuku hiyo.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.
WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.
https://1.bp.blogspot.com/-beysvs3frjg/V8byeVULdFI/AAAAAAAAN2E/93WVxRmKnW4Xyl-GpJPMWdv8L97kWW3BwCLcB/s640/1.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-beysvs3frjg/V8byeVULdFI/AAAAAAAAN2E/93WVxRmKnW4Xyl-GpJPMWdv8L97kWW3BwCLcB/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/watetezi-wa-haki-za-binadamu-nchini.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/watetezi-wa-haki-za-binadamu-nchini.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago