Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa ya UTEUZI Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli afanya uteuzi wa Katibu Tawala Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri 13

     Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Se...


   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
-

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2016 amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.

Bw. Eliya Mtinangi Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana tarehe 09 Septemba, 2016 ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Bw. Tixon Tuliangine Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1.      Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa ya Dodoma
2.      Elias R. Ntiruhungwa             - Mji wa Tarime
3.      Mwantumu Dau                     - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
4.      Frank Bahati                          - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
5.      Hudson Stanley Kamoga        - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
6.      Mwailwa Smith Pangani         - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
7.      Godfrey Sanga                       - Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
8.      Yusuf Daudi Semuguruka      - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
9.      Bakari Kasinyo Mohamed     - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
10.   Juma Ally Mnwele                 - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
11.   Butamo Nuru Ndalahwa       - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
12.   Waziri Mourice                    - Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
13.   Fatma Omar Latu                 - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo


Wakurugenzi wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne tarehe 13 Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam10 Septemba, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa ya UTEUZI Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli afanya uteuzi wa Katibu Tawala Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri 13
Taarifa ya UTEUZI Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli afanya uteuzi wa Katibu Tawala Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri 13
https://1.bp.blogspot.com/-ls5N8IEyft0/V9PtIAfCZhI/AAAAAAADjb8/FpLpZqB06cA_iTAvOq4jD9Qssx1QHYDtACLcB/s640/IMGS0012.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-ls5N8IEyft0/V9PtIAfCZhI/AAAAAAADjb8/FpLpZqB06cA_iTAvOq4jD9Qssx1QHYDtACLcB/s72-c/IMGS0012.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/taarifa-ya-uteuzi-kutoka-ikulurais-dr.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/taarifa-ya-uteuzi-kutoka-ikulurais-dr.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago