Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZULU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa  Makamu wa Rai...  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba


 
Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli akiomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
 -
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani hapa.


Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo katika Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezulu Kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.

Akizungumza mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.

"Mimi najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa uvumilivu na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pemba
02 Septemba, 2016


COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZULU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA
RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZULU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA
https://4.bp.blogspot.com/-U1cezRD7A7I/V8mPGWU122I/AAAAAAADjVk/XAHjfS43Eb8Ak1S3vmuSZDXmYjX6BSHAgCLcB/s640/14233089_10209084262416741_7813970947157580184_n.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-U1cezRD7A7I/V8mPGWU122I/AAAAAAADjVk/XAHjfS43Eb8Ak1S3vmuSZDXmYjX6BSHAgCLcB/s72-c/14233089_10209084262416741_7813970947157580184_n.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/rais-dkt-john-pombe-magufuli-na-mkewe.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/rais-dkt-john-pombe-magufuli-na-mkewe.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago