Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI ENG. RAMO MAKANI AONANA NA VIONGOZI NA WADAU WA RAFIKI WILDLIFE FOUNDATION KUZUNGUMZIA KAMPENI YA KUPIGA VITA UJANGILI NCHINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani (kushoto) akizunumza na viongozi na wadau shirikishi wa  Shirika lisilo l...

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani (kushoto) akizunumza na viongozi na wadau shirikishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Rafiki Wildlife Foundation kuhusu Kampeni ijulikanayo kama "Jitokeze Tuongee, Piga Vita Ujangili Afrika na Wizara ya Maliasili na Utalii" iliyoandaliwa na shirika hilo kwa ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wengine ofisini kwake Dar es Salaam jana, tarehe 21 Septemba, 2016. Kampeni hiyo imepangwa kuzinduliwa Jijini Arusha tarehe 07 Oktoba, 2016. Kulia ni mdau wa kampeni hiyo ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Viti Maalum , Al-Shaymaa Kwegyir.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na viongozi na wajumbe shirikishi wa Rafiki Wildlife Foundation ofisini kwake jana. Alieleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kupiga vita ujangili na kuimarisha uhifadhi wa Maliasili nchini. Alitoa wito kwa watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao na kupenda Malisili za taifa na kujenga utaratibu wa kuzitembelea ili kukuza utalii wa ndani ambao Wizara imejipanga kuuendeleza kuhakikisha unakuwa kwa kasi ili kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa.
 Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Rafiki Wildlife Foundation, Mchungaji Clement Matwiga (wa tatu kulia) akizungumza katika kikao hicho, Mchungaji huyo alitoa wito kwa watanzania kuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa wanyamapori hususani Tembo na Faru kwa kuwa wana faida kubwa kwao kiuchumi na kijamii, alisema kuwa kwa sasa jamii inaona  jukumu hilo ni la Serikali pekee kupitia Wizara ya Maliasili na Taasisi zake jambo ambalo sio sahihi. Akielezea kuhusu kampeni ya "Jitokeze Tuongee, Piga Vita Ujangili Afrika na Wizara ya Maliasili na Utalii"  itakayozinduliwa Jijini Arusha na Waziri wa Maliasili na Utalii alisema, itahusisha fursa mbalimbali ikiwemo kutembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa ndani, Semina mbalimbali kuhusu uhifadhi pamoja na michezo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wajumbe shirikishi wa Rafiki Wildlife Foundation ofisini kwake jana.
(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii - www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: NAIBU WAZIRI WA MALIASILI ENG. RAMO MAKANI AONANA NA VIONGOZI NA WADAU WA RAFIKI WILDLIFE FOUNDATION KUZUNGUMZIA KAMPENI YA KUPIGA VITA UJANGILI NCHINI
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI ENG. RAMO MAKANI AONANA NA VIONGOZI NA WADAU WA RAFIKI WILDLIFE FOUNDATION KUZUNGUMZIA KAMPENI YA KUPIGA VITA UJANGILI NCHINI
https://4.bp.blogspot.com/-DOLMLkkcWPc/V-Ka6Z41vjI/AAAAAAAAHjc/wh14GSo5_8I85757qZ5KM1S-qWoZqIxBgCLcB/s640/DSC_7511.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-DOLMLkkcWPc/V-Ka6Z41vjI/AAAAAAAAHjc/wh14GSo5_8I85757qZ5KM1S-qWoZqIxBgCLcB/s72-c/DSC_7511.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/naibu-waziri-wa-maliasili-eng-ramo.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/naibu-waziri-wa-maliasili-eng-ramo.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago