Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKURUGENZI ILEJE HAJI MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mit... Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa  kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.
baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.


Na fredy mgunda,ileje

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.
Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.
“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.
Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi  wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.
Lakini mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKURUGENZI ILEJE HAJI MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA
MKURUGENZI ILEJE HAJI MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA
https://3.bp.blogspot.com/-wYxbDmh8U-s/V83TDZQM24I/AAAAAAAACS4/a04VC4KRZ_4Uk50rXRNMhfrCvgQ6tKy5QCLcB/s640/IMG-20160905-WA0162.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-wYxbDmh8U-s/V83TDZQM24I/AAAAAAAACS4/a04VC4KRZ_4Uk50rXRNMhfrCvgQ6tKy5QCLcB/s72-c/IMG-20160905-WA0162.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/mkurugenzi-ileje-haji-mnasi-atoa-onyo.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/mkurugenzi-ileje-haji-mnasi-atoa-onyo.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago