Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MeTL Group yafanya uzinduzi wa kampeni ya “USIKATE TAMAA”

  Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akielezea kampeni ya USIKATE TAMAA na jinsi inavyoweza kubadili maisha ya wat...


 Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akielezea kampeni ya USIKATE TAMAA na jinsi inavyoweza kubadili maisha ya watu waliokata tamaa ya kufanikiwa kimaisha.kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidiz wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
 Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumza kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige. 
  Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki hadi kufika hatua aliyopo sasa ambayo mwenyewe amesema kuwa kwake ni mafanikio makubwa. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer. kulia na Kaimu Meneja Masoko Msaidizi wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akiwa katika picha ya pamoja na Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta, kuashiria kuwa kampeni ya USIKATE TAMAA imezinduliwa rasmi.


Kwa kutambua hali ambayo inawakuta watu wengi katika jamii na kupoteza matumaini ya kufanikiwa kimaisha, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.
Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.
Alisema kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali na sasa wamefanikiwa kimaisha.
“Kuna watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.
Mkurugenzi wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.
“MeTL kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu zaidi,” alisema Fatema.
Kwa upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.
“Unaweza kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi nifanye hivyo,
“Ilikuwa naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MeTL Group yafanya uzinduzi wa kampeni ya “USIKATE TAMAA”
MeTL Group yafanya uzinduzi wa kampeni ya “USIKATE TAMAA”
https://2.bp.blogspot.com/-iDtZanr0COc/V9gDvsfz1MI/AAAAAAABmaA/tyuRmqdmO0ACitzpAtzo0Sc7WSgjMNkDACLcB/s640/Fatema%2B1.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-iDtZanr0COc/V9gDvsfz1MI/AAAAAAABmaA/tyuRmqdmO0ACitzpAtzo0Sc7WSgjMNkDACLcB/s72-c/Fatema%2B1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/metl-group-yafanya-uzinduzi-wa-kampeni.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/metl-group-yafanya-uzinduzi-wa-kampeni.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago