Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULU ASEMA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA NI IMARA, ASEMA "WAPIGA DILI" WAMEDHIBITIWA

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Museum wa ...Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Museum wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016 kuhusu hali ya uchumi wa taifa. (PICHA NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, amesema hali ya uchumi wa Tanzania ni ya kuridhisha tofauti na taarifa zinazozagaa kuwa uchumi wa nchi umedorora.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Museum wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016, Gavana huyo alisema, hali ya uchumi ni imara kwa vile tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano, mfumuko wa bei umedhibitiwa na unashuka siku hadi siku hali kadhalika, thamani ya shilingi nayo inaendelea kuimarika.
Profesa Ndulu pia alisema,si kweli kwamba, fedha zimepungua mitaani bali fedha zipo ila fedha za “dili”ni kweli “zimekauka” na hii ni kutokana na jitihada za serikali katika kuziba mianya ya rushwa, wakwepa kodi na matumizi mabaya fedha za umma.
Aliwatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa, hali ya uchumi wetu itaendelea kuimarika katika mwaka 2016 kutokana na viashiria kadhaa ambavyo ni pamoja na uzalishaji wa umeme katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, umeongezeka kwa asilimia 14.5 kufikia KwH milioni  3,454.2 ikilinganishwa na na kWh milioni 3,016.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Akifafanua zaidi alisema, ongezeko hilo la umeme limetokana na jitihada za serikali katika kutumia nishati ya gesi kwenye uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi I. “Umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia 52.2, hali itakayosaidia kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na sekta nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na hivyo kuchangia katika kuongeza pato la Taifa na pia ghjarama ya umeme itashuka.” Alisema.
“Kumekuwepo na taarifa nyingi zinazozagaa kuwa uchumi umedorora, lakinikwanza napenda niweke wazi, mimi si mwanasiasa, mimi nataka kulizungumzia swala hili kitaalamu, ukiangaliatakwimu za Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuajiwa uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha, katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka  kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015, sasa kwa takwimu hizi hauwezi kusema uchumi umedorora, hii si kwelikabisa,” alisema Profesa Ndulu.
Taarifa kamiliya Profesa Benno Ndulu kuhusu hali ya uchumi soma hapo chini.

Profesa Ndulu na wasaidizi wake kutoka kushoto, Meneja Uhusiano na masuala ya peotokali, Zaria K. Mbeo, Mkurugenzi wa Sera na Uchumi, Johnson Nyela, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kened A. Nyoni, wakinakili maswali toka kwa waandishi wa habari
 Profesa Ndulu akizungumza
Bibi Mbeo

Taarifa ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu kwa Waandishi wa habari hii hapa chini

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULU ASEMA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA NI IMARA, ASEMA "WAPIGA DILI" WAMEDHIBITIWA
GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULU ASEMA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA NI IMARA, ASEMA "WAPIGA DILI" WAMEDHIBITIWA
https://4.bp.blogspot.com/-v6ooBqbRdhQ/V9kohFMBGKI/AAAAAAAAswY/3G4LM9-hPuEi5WDZDIEyUoP_GaUkcL4oACLcB/s640/5R5A1909.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-v6ooBqbRdhQ/V9kohFMBGKI/AAAAAAAAswY/3G4LM9-hPuEi5WDZDIEyUoP_GaUkcL4oACLcB/s72-c/5R5A1909.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/gavana-wa-benki-kuu-ya-tanzania-profesa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/gavana-wa-benki-kuu-ya-tanzania-profesa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago