Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

DC WA HANDENI,MH GONDWE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUTI KWA WACHIMBAJI WADINI WASIOKUWA NA LESENI

Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh.Gondwe akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ...


Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh.Gondwe akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni, pembeni ni Afisa madini mkazi Bw. makiyao akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa.

 Mmoja wa wataalamu wa madini akitoa ufafanuzi kidogo kwa wachimbaji wadogo wa madini wilayani handeni
 Baadhi ya wachimbaji madini wadogo waliohudhuria kikao hicho


Na Alda Sadango,Afisa Habari wilaya ya Handeni.

Mkuu wa wilaya ya Handeni MH. Gondwe amepiga marufuku matumizi ya baruti kwa wachimbaji wa madini wasiokua na leseni, amesema hayo kwenye kikao cha wachimbaji madini wadogo kilichoandaliwa na afisa madini mkazi Bw. Makyao jana.

Amewaeleza wachimbaji kwamba matumizi ya baruti kinyume na taratibu yanaweza kuleta hatari na madhara kwenye suala zima la usalama. 
"Nimewapa mamalaka wachimbaji walio na leseni kwa sababu ni kama kitendea kazi kwao lakini pia wanatumia kwa kufuata sheria taratibu na kanuni, Afisa madini mkazi atasimamia magari yanayochukua baruti, kuhakiki maeneo yanayotunzwa baruti hizo na kuhakiki matumizi sahihi ya baruti hizo kabla ya kwenda kuchukua baruti nyingine",alisema DC Gondwe

Alisema kuwa kumekuwepo na ulipuaji wa baruti uliokithiri kwa wachimbaji wasiokua na leseni, hali ambayo imekuwa ikipekelea matatizo ya hapa na pale katika mfumo mzima wa kiutendaji. Mh.Gondwe amewapa muda hadi kufikia Oktoba  13,2016 wawe wamepata leseni za uchimbaji kihalali na kwamba baada ya hapo itaendeshwa oparesheni ya kuwakamata wasiokua na leseni na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema Sheria ya madini inatambulika na adhabu za makosa hayo ni kulipa kiasi cha Milioni 5, kufungwa jela miaka3 au vyote kwa pamoja.Na yeye kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama atahakikisha anasimamia hilo kwa maana inakosesha hata serikali mapato kwa kukwepa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kwa kipindi tangu 2014 hadi sasa serikali imepoteza kiasi cha 5.1 bilioni ambapo ni sawa na 1.7 bilioni kila mwaka,hivyo kuna watu wana leseni halali tangu 2014 lakini wameshindwa kuanza kazi kwa sababu ya watu wasiokua na leseni kuwepo maeneo hayo.

Amewaomba wachimbaji wadogo hao ambao wanafuata sheria taratibu na kanuni kushirikiana na uongozi wa wilaya kuhakikisha kwamba wanadhibiti matumizi yasiyo halali ya baruti na wanaokwepa kulipa kodi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: DC WA HANDENI,MH GONDWE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUTI KWA WACHIMBAJI WADINI WASIOKUWA NA LESENI
DC WA HANDENI,MH GONDWE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUTI KWA WACHIMBAJI WADINI WASIOKUWA NA LESENI
https://4.bp.blogspot.com/-0CN65vS6DKI/V-OTyIhYwgI/AAAAAAADUA4/5LeQoQkNaEco5z6pX3C9EDzyqZ6u7nOIgCLcB/s640/index.jpeg
https://4.bp.blogspot.com/-0CN65vS6DKI/V-OTyIhYwgI/AAAAAAADUA4/5LeQoQkNaEco5z6pX3C9EDzyqZ6u7nOIgCLcB/s72-c/index.jpeg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/09/dc-wa-handenimh-gondwe-apiga-marufuku.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/09/dc-wa-handenimh-gondwe-apiga-marufuku.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago