Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki afanya kikao kazi na watumishi wa ofisi yake

 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi w...

 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha robo  mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kulia) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.Katikati ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akisikiliza kwa makini.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo  mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi Bw. Kamugisha Rufulenge.
 Mtumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Victor Kitu (aliyesimama) akiwasilisha malalalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
--
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wadau ili kujenga taswira nzuri ya Ofisi hiyo.
Mhe. Kairuki aliyasema hayo wakati wa kikao kazi cha robo mwaka na watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Alisema, Ofisi ya Rais – Utumishi kama jina lenyewe lilivyo, inatakiwa kuwa kioo na mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali kwa kutoa huduma bora  na kwa wakati kwa wadau wake.

Mhe. Kairuki aliwataka watumishi hao kuangalia ni kwa jinsi gani huduma wanazotoa kwa wadau zinazingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utumishi wa umma.

“Tutoe huduma kwa kuzingatia taratibu zilizopo na uadilifu mkubwa,”  Mhe. Kairuki alisisitiza.

Aliongeza kuwa, wapo baadhi ya watumishi wana majibu ya hovyo sana kwa wateja, hivyo aliahidi  kuwafuatilia, na iwapo wakibainika hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa dhidhi yao.

Aidha, Mhe. Kairuki aliwataka watumishi hao kuwa na utamaduni wa   kujisomea na kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo wanayoyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

“Wapo baadhi ya watumishi hawana utamaduni wa kujisomea, wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na matokeo yake hujikuta wakishindwa kufanya inavyopaswa.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Mhe. Kairuki amejiwekea utaratibu wa kukutana na watumishi wa ofisi yake kila robo mwaka kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutumishi na kiutendaji.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki afanya kikao kazi na watumishi wa ofisi yake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki afanya kikao kazi na watumishi wa ofisi yake
https://1.bp.blogspot.com/-vOi6pQq2L_8/V6n5zz_TzBI/AAAAAAADiwA/P0pCjPh2ACI063xKMLZzWhWK3AfF-mjCACLcB/s640/jav3-768x512.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-vOi6pQq2L_8/V6n5zz_TzBI/AAAAAAADiwA/P0pCjPh2ACI063xKMLZzWhWK3AfF-mjCACLcB/s72-c/jav3-768x512.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/waziri-wa-nchi-ofisi-ya-rais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/waziri-wa-nchi-ofisi-ya-rais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago