Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Utashi wa Rais Magufuli suluhisho la vifo vinavyotokana na uzazi nchini

Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay (katikati) akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria...


Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay (katikati) akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina juu ya namna ya mamlaka husika kukabiliana na matukio ya vifo vinavyotokana na uzazi. Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay (katikati) akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina juu ya namna ya mamlaka husika kukabiliana na matukio ya vifo vinavyotokana na uzazi.Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Sizarina Hamisi (kushoto) akiwasilisha mada katika semina hiyo kwa wanahabari. Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Sizarina Hamisi (kushoto) akiwasilisha mada katika semina hiyo kwa wanahabariOfisa Habari wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo. Ofisa Habari wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo.Chiku Lweno (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ). Chiku Lweno (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama

----  IMEELEZWA kwamba utashi wa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na moyo wa huruma atakaouonesha juu ya matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi ni suluhisho la kudumu la janga la vifo hivyo ambavyo kila siku vimekuwa vikipoteza maisha ya mama na mtoto. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay kwenye semina kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni kuwajengea uwezo wanahabari hao kupaza sauti juu ya kukabiliana na vifo vinavyotokana na uzazi kwa wajawazito. 

Bi. Mlay alisema endapo Rais Magufuli atatamka kuanzia leo kuwa hataki kusikia matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi vinaweza kudhibitiwa na vikatokomea. Alisema vifo hivyo vinaweza kuzuilika endapo akinamama wote wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za uzazi za dharura kwa wakati na wataalamu stahiki. "...Nasema hivyo kwa sababu Mh. Rais akitamka leo hii kwamba kuanzia leo hataki kusikia kifo hata kimoja cha mwanamke kinatokea kutokana na matatizo ya uzazi, basi itakuwa hivyo. Hii ni kwa sababu vifo hivi vinazuilika kama kinamama wote wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za uzazi za dharura ni jambo muhimu hapa kwa sababu matatizo yanayosababisha vifo hayasubiri," alisema Bi. Mlay. 

Alisema takwimu zinaonesha kwa kila uchao takribani akinamama 24 wanakufa kwa matatizo ya uzazi nchini kwa kile kukosa huduma kamili za uzazi za dharura stahiki, jambo ambalo linaweza kudhibitiwa endapo maamuzi yatafanywa na mamlaka husika. Aidha Mratibu huyo wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama alieleza hali hiyo inaweza kudhibitiwa endapo wilaya zote zinatoa kipaumbele na kutenga fungu pekee la huduma kamili za uzazi za dharura na kuzilinda kuhakikisha zinatumika kwa makusudio yaliyowekwa. Bajeti za halmashauri zitumwe kwa wakati mara zinapopitishwa ili ziweze kutumika kwa wakati na kutatua changamoto hizo. bajeti kwa wakati na wataalamu stahiki.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Utashi wa Rais Magufuli suluhisho la vifo vinavyotokana na uzazi nchini
Utashi wa Rais Magufuli suluhisho la vifo vinavyotokana na uzazi nchini
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/08/IMG_1827.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/utashi-wa-rais-magufuli-suluhisho-la.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/utashi-wa-rais-magufuli-suluhisho-la.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago