Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA LINDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa ...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kagwa.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Godfrey Zambi akisoma taarifa ya mkoa wakati wa mkutano uliowakutanisha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Andrea Kagwa.

Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi waliohudhuria mkutano wao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu 
---
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wa mkoa wa Lindi wasimamie kikamilifu zoezi la utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha madawati yanayotengenezwa yanakuwa na ubora na yanakidhi viwango vinavyotakiwa


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Lindi Tarehe  7-Aug-2016 katika mkutano wake na wajasiriamali wa mkoa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.


Makamu wa Rais amesema msukumo mkubwa wa serikali uliopo kwa sasa unalenga kuhakikisha madawati yanayotengenezwa kote nchini yanakuwa imara  huku akipongeza  jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya mkoa wa Lindi ya utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa mkoa huo umebakisha asilimia Moja tu ya utengenezaji wa madawati hayo ili kukamilisha zoezi hilo.


Kuhusu mikopo kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali italifanyia kazi ombi la wajasiriamali wa mkoa wa Lindi ambao wameiomba serikali ifanye mazungumzo na watendaji wa taasisi za kifedha nchini ili waweze kupunguza riba kwenye mikopo wanayopata kama hatua ya kuongeza hamasa kwa wananchi wengi zaidi kukopa fedha kwa ajili ya kuimarisha shughuli ujasiriamali.


Makamu wa Rais pia amezitaka halmashauri zote nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kutenga asilimia TANO ya makusanyo ya mapato yake na kutoa fedha hiyo kwa wanawake na vijana kwenye halmashauri hizo ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi yao ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA LINDI
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA LINDI
https://1.bp.blogspot.com/-J09CxjJJv0U/V6fswvI6HpI/AAAAAAAAySw/2y3wIqy3hXgsOxSCHGZaiRSxTfb5axnKQCEw/s640/12.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-J09CxjJJv0U/V6fswvI6HpI/AAAAAAAAySw/2y3wIqy3hXgsOxSCHGZaiRSxTfb5axnKQCEw/s72-c/12.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-akutana.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-akutana.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago