Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KAMPUNI YA STATE GRID YAONESHA NIA MRADI WA UMEME WA MCHUCHUMA- MAKAMBAKO

  Waziri wa Nishati na Madini (katikati) Profesa Sospeter Muhongo akiwaeleza jambo Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza ...

 Waziri wa Nishati na Madini (katikati) Profesa Sospeter Muhongo akiwaeleza jambo Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni hiyo inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati nchini.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya State Grid ya China upande wa Afrika, Mingu Liu, (wa kwanza kulia mbele) wakati akimweleza Waziri Muhongo azma ya Kampuni hiyo kuwekeza katika Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kV 400 Mchuchuma hadi Makambako. Wengine wanaofuatilia ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na ujumbe wake.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao baina yake na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni ya State Grid ya China inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati nchini
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiangalia Makabrasha kutoka Kampuni ya State Grid ya China ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa njia ya umeme ya Msongo wa kV 400 ya Mchuchuma hadi Makambako.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikakti) na Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youging (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Waziri, Balozi na kampuni ya State Grid. 
-
 
Kampuni ya State Grid ya China imeonesha nia ya kuwekeza katika Mradi wa Kujenga Njia ya umeme ya Msongo wa kV 400 ya kutoka Mchuchuma hadi Makambako.

Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing aliyeambatana na ujumbe huo wa kampuni hiyo.

Profesa Muhongo alichukua fursa hiyo kuieleza kampuni hiyo kuhusu Hazina iliyopo nchini ya Makaa ya Mawe na kusema kuwa, bado Serikali inatafuta wawekezaji ambao watazalisha umeme kwa kutumia chanzo hicho na kuongeza kuwa, “Bado tunahitaji wawekezaji kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe”.

Aidha, mbali na kuonesha nia ya kuwekeza katika Mradi huo, Kampuni hiyo imefika Wizarani kutaka kujua maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya Nishati ambayo kampuni hiyo inaweza kufanya kazi nchini.

Vilevile, kampuni hiyo ilimweleza Waziri uzoefu ilionao katika shughuli hizo na kuzitaja baadhi ya nchi ambazo inatekeleza miradi kama hiyo kuwa barani Afrika kuwa ni pamoja na Ethiopia, Egypt, Kenya na Afrika Kusini.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KAMPUNI YA STATE GRID YAONESHA NIA MRADI WA UMEME WA MCHUCHUMA- MAKAMBAKO
KAMPUNI YA STATE GRID YAONESHA NIA MRADI WA UMEME WA MCHUCHUMA- MAKAMBAKO
https://2.bp.blogspot.com/-8j9801pLBDQ/V711mr1rM4I/AAAAAAADjG8/siJo_gC3CngK2MwEyfdBIBa2UXVXnc55ACLcB/s640/State%2BGrid%2B1.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-8j9801pLBDQ/V711mr1rM4I/AAAAAAADjG8/siJo_gC3CngK2MwEyfdBIBa2UXVXnc55ACLcB/s72-c/State%2BGrid%2B1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/kampuni-ya-state-grid-yaonesha-nia.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/kampuni-ya-state-grid-yaonesha-nia.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago