Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Bodi ya Filamu yatoa siku 7 kwa Pamoja Film Company kuwasilisha nyaraka za kazi zao

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo akionyesha moja ya nyaraka zilizokiukwa na Kampuni ya Usambazaji wa Filamu nchin...

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo akionyesha moja ya nyaraka zilizokiukwa na Kampuni ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Pamoja Film Company wakati wa kikao baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na kampuni hiyo ya usambazaji wa filamu. Bi Fisoo amewaasa wadau wa filamu kufuata sheria na kanuni zinazoongoza sekta ya filamu nchini. 
 ---
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO 
Bodi ya Filamu Tanzania imetoa siku saba kwa Kampuni ya Usambazaji wa Filamu ijulikanayo kama ‘Pamoja Film Company’ kuwasilisha nyaraka za filamu zake ili kukagua na kuhakikisha kama wamefuata sheria na kanuni zinazosimamiwa na bodi hiyo. Hatua hiyo imefikiwa baada ya kampuni hiyo kubainika kukiuka baadhi ya sheria na kanuni za usambazaji zikiwemo za kutowasilisha miswada ya filamu (script) kabla ya kuanza kurekodi, kuzitangaza kazi hizo kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuzifikisha Bodi ya Filamu Tanzania Kwa ajili ya ukaguzi pamoja na kufanya kazi za utengenezaji na usambazaji wa filamu bila kibali. Agizo hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Lufingo Exaud kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa kukiuka sheria na kanuni zinazosimamiwa na bodi ni kosa kisheria.

 “Natoa siku saba kwa Kampuni hii kuwasilisha miswada ya filamu zake 12 alizozitangaza na kuzisambaza kinyume cha sheria pamoja na kuleta maelezo kwa maandishi ya kujieleza sababu zilizowapelekea kufanya kazi hizo bila kibali kutoka bodi”,alisema Fissoo. Filamu hizo zilizotolewa na Kampuni hiyo bila kufuata sheria na kanuni ni; Spompompo, Tanga Raha, Buku 10, Jirani Hafugiki, Mke Sahihi, Chanzo, Ahsante, Je Alaumiwe, Mwaka wa Tisa, Nyaraka na Kanya Boya. Fisoo ameongeza kuwa Bodi imefanya jitihada kubwa kutoa elimu kwa umma kupitia njia za vipeperushi,

 kuandaa na kushiriki mikutano na makongamano ya kitaifa na kimataifa, kushiriki maonesho na maadhimisho ya kisekta na kitaifa ikiwa na lengo la kuwaelemisha wadau wa filamu kuhusu sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta hiyo nchini. Aidha, amewaonya wadau wote wa filamu kuacha kukiuka sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa kisheria, “tunawaonya wadau wote kuacha mara moja tabia hii” alimalizia. Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lufingo Exaud amekiri makosa yake na ameahidi kulipa faini za makosa yote, pia ameomba msamaha mbele ya Bodi hiyo na kuapa kuwa hatorudia tena. 

Kwa kumalizia ameahidi kuwa balozi mzuri wa Bodi ya Filamu Tanzania na yupo tayari kuwapa elimu wadau wengine wa filamu nchini ili waweze kufuata sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo. Mbali na kuahidi kushirikiana na bodi hiyo, Lufingo ameusifia utaratibu wa bodi wa kurahisisha upatikanaji wa vibali kwani kwa sasa baada ya kuwasilisha muswada wa filamu kwa ajili ya ukaguzi utapatiwa kibali ndani ya muda wa siku saba za kazi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Bodi ya Filamu yatoa siku 7 kwa Pamoja Film Company kuwasilisha nyaraka za kazi zao
Bodi ya Filamu yatoa siku 7 kwa Pamoja Film Company kuwasilisha nyaraka za kazi zao
https://3.bp.blogspot.com/-C0_2CLpZayo/V7cOqxP5SxI/AAAAAAADi5Q/Unf49xRocn86JPGoCRwgKLCMR9-ae91pQCLcB/s640/IMG_0103.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-C0_2CLpZayo/V7cOqxP5SxI/AAAAAAADi5Q/Unf49xRocn86JPGoCRwgKLCMR9-ae91pQCLcB/s72-c/IMG_0103.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/bodi-ya-filamu-yatoa-siku-7-kwa-pamoja.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/bodi-ya-filamu-yatoa-siku-7-kwa-pamoja.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago