Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Balozi Mpya (Mteule) wa Uingereza awasili Dar es Salaam

Bi. Sarah Cooke Balozi Mteule wa Uingereza Dar es Salaam – Tanzania  ----- Balozi Mpya (Mteule) wa Uingereza a...

Bi. Sarah Cooke Balozi Mteule wa Uingereza Dar es Salaam – Tanzania
 -----
Balozi Mpya (Mteule) wa Uingereza awasili Dar es Salaam

Bibi Sarah Cooke, Balozi mpya (Mteule) wa Uingereza nchini Tanzania awasili jana 25 Agosti, 2016 Dar es Salaam

Bi.Cooke amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi.Dianna Melrose (ambaye amestaafu) na ni mwanamke wa tatu kushika nyadhifa ya ubalozi kuiwakilisha Uingereza nchini Tanzania.
Bi Cooke alijiunga na Utumishi Uingereza mnamo mwaka 2002. Alifanya kazi kadha wa kadha katika idara za Serikali ya Uingereza ikiwemo Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Wizara ya Mambo ya Nje na Kitengo cha Mikakati cha Waziri Mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri. Pia alipata kuhudumu kama Makamu Mkuu wa Tume ya Sekretariati ya Africa. Hivi karibuni, alikuwa ndiye Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (DFID) nchini Bangladesh. Kabla ya kujiunga Utumishi katika Serikali ya Uingereza, alipata kufanya kazi kama Mchumi jijini London, Guyana na visiwa vya Solomoni.
Juu ya uteuzi wake, Bi.Cooke alisema;

“Nimefurahi na ni heshima kubwa kwangu kupewa jukumu hili jipya kama Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Uingereza na Tanzania inafurahia mahusiano na ushirikiano wa muda mrefu na kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ambayo tunashabihiana katika vipaumbele ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo na usalama. Nina dhamiria kuimarisha ushirikiano huu bora zaidi na nina taraji kuijua vyema Tanzania na watu wake”

Taarifa zaidi kwa wahariri:
  • Mabalozi wa Uingereza Wanawake waliopata kuhudumu Tanzania ni pamoja na; Dianna Melrose (2013-2016) na Diane Corner (2009-2012)
  • Tume ya Afrika ilianzishwa mapema 2004 kama mshauri wa Serikali ya Uingereza juu ya Masuala yahusuyo G8 ambapo Uingereza ilikuwa Rais wa kundi hilo (G8) mwaka 2005. Tume ilikuwa na wajumbe 17 akiwemo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. Ripoti ya Tume hiyo, “Vipaumbele vyetu vinavyoshabihiana” ilipendekeza hatua ambazo zitumike kujenga na kustawisha Afrika. Mengi ya mapendekezo hayo yalichukuliwa na kundi la G8 mnamo mwaka 2005 na katika maazimio mengine makubwa ya Afrika na Kimataifa.

Kwa mawasiliano zaidi;

Michael Dalali,
Afisa Miradi na Habari,
Ubalozi wa Uingereza, Dar es Salaam
Simu: +255 (0) 22 229 0269
Simu: +255 (0)762 791 991

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Balozi Mpya (Mteule) wa Uingereza awasili Dar es Salaam
Balozi Mpya (Mteule) wa Uingereza awasili Dar es Salaam
https://1.bp.blogspot.com/-w1tOmCjaMng/V8BnBvJzP9I/AAAAAAADjNc/d6zGLe1-T6M58VF_tbG2u_fvoWmjwDEcgCLcB/s640/Sarah%2BCooke%2BA.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-w1tOmCjaMng/V8BnBvJzP9I/AAAAAAADjNc/d6zGLe1-T6M58VF_tbG2u_fvoWmjwDEcgCLcB/s72-c/Sarah%2BCooke%2BA.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/08/balozi-mpya-mteule-wa-uingereza-awasili.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/08/balozi-mpya-mteule-wa-uingereza-awasili.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago