Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MADARASA YA SEKONDARI YA LINDI YALIYOUNGUA MOTO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara na madarasa yaliyoungua kwa moto katika shule ya sekondari ya Lindi akiwa katika zi...


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara na madarasa yaliyoungua kwa moto katika shule ya sekondari ya Lindi akiwa katika ziara ya mkoa huo Julai 14, 2016  Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na  mkewe Mary wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nangumbu wilayani Luangwa baada ya kuwasili kijijini hapo wakiwa katika ziara ya mkoa wa Lindi  Julai 14, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. 

Mke wa Waziri Mkuu, Mama  Mary Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangumbu wilayani Luangwa ambako ameambatana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ziara ya mkoa wa Lindi, Julai 14, 2016.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nangumbu wilayani Luangwa  baada ya kuwasili kijijini hapo ili kuzungumza na wananchi wakiwa katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 14, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
-
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaahidi Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lindi kwamba Serikali itahakikisha miundombinu iliyoungua moto inakarabatiwa kwa haraka ili shughuli za masomo ziweze kuendelea kama awali.

Pia amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili (Julai 17, 2016) katika harambee ya kuchangia ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo leo (Alhamisi Julai 14,2016) wakati alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kujionea athari zilizosababishwa na moto uliotokea usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu na kuunguza vyumba tisa vya madarasa.

“Mkoa tayari umeshafanya tathimini ya athari zilizobabishwa na moto huo hivyo naomba tuletewe taarifa ya tathmini hiyo ya uharibifu wote pamoja na gharama zinazohitajika ili tuhakikishe miundombiunu hii inarudi na shughuli ziweze kuendelea kama awali,” amesema.

“Nawaomba walimu na watumishi wengine shuleni hapa kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya na kwamba Serikali itarudisha miundombinu iliyoharibika kwa haraka,” alisema.Akisoma taarifa ya ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alisema chanzo cha moto huo ni kutokea kwa tatizo la umeme kwenye chumba cha ofisi ya walimu.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema maafa hayo yameathiri shule hiyo kwa asilimia 34 na kusababisha hasara ya sh. milioni 682.78.“Moto huu umetokea siku moja kabla ya kufunguliwa kwa shule.Uongozi wa Mkoa unaendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo inarudi katika hali yake ya kawaida,” alisema.

Zambi alitaja miundombinu mingine iliyoathirika na moto huo kuwa ni jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia ambalo litahitaji upauaji upya baada ya paa lake kuteketea kwa moto. 

Alisema kwa sasa masomo yanaendelea kama kawaida shuleni hapo ambapo wanafunzi wanasomea katika bwalo la chakula pamoja na kwenye chumba cha maabara cha baiolojia. 

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMISI, JULAI 14, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MADARASA YA SEKONDARI YA LINDI YALIYOUNGUA MOTO
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MADARASA YA SEKONDARI YA LINDI YALIYOUNGUA MOTO
https://4.bp.blogspot.com/-nRR_rsiDA7c/V4eJ8QqVU6I/AAAAAAADidw/eqn2ARncV-wSDtDrnckFXCskBKZPkJ7dQCLcB/s640/IMGS5703.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-nRR_rsiDA7c/V4eJ8QqVU6I/AAAAAAADidw/eqn2ARncV-wSDtDrnckFXCskBKZPkJ7dQCLcB/s72-c/IMGS5703.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-akagua.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-akagua.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago