Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WANAHABARI JIJINI MWANZA WAMLILIA MAREHEMU MWALIMU SOKORO, ALIEKUWA MHARIRI WA BARMEDAS TV.

Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa Barmedas Tv ya Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki ...


Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa Barmedas Tv ya Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Kifo chake kimesababisha majonzi makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waandishi wa habari Jijini Mwanza ambao baadhi yao walipitia mikono ya Sokoro aliefahamika kwa jina maarufu la Mwalimu kutokana na ujuzi wake katika kufundisha nyimbo za Injili na ubobeaji wake katika taaluma ya habari.

Enzi za uhai wake alikuwa Mwalimu wa kwanza wa Kwaya ya AICT Makongoro waliowahi kutamba na wimbo wa Kekundu huku pia akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza katika kituo cha luninga cha Barmedas Tv Cable ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa njia ya cable tu kabla ya hivi karibuni kupatikana katika ving'amuzi mbalimbali.

Mwalimu Charles Sokoro alizaliwa mwaka 1965 na mauti yamemfika mwaka huu 2016 akiwa na miaka 51. Ratiba ya Mazishi ni kama ifuatavyo;

1.Siku ya Jumatatu (18/7/2016 )  saa 10:00 jioni, Mwili wa Marehemu kuwasili kutoka hospitalini Bugando kuelekea Kanisa La AICT Makongoro

2.Siku ya Jumanne (19/7/2016) Kanisa La AICT Makongororo
~Saa 6:00 mchana IBADA ya Kumuaga Mareemu

~Saa 7:30 mchana Safari ya kuelekea Malaloni (Makaburini Kitangiri )

~Saa 8:30 Chakula na baadaye kuhitimisho.
Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake
Wanahabari Mwanza wakieleza namna wavyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.

Ni juzi tu Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba mwingine wa kaka yetu sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha midomo wazi tunahisi km ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.

Nani asiye mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli  alikuwa mcheshi asiye na makuu.
Aliipenda taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.

Hakuonyesha umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani asiyejua uwezo wake.kwenye kupiga kinanda?.

Nani asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?
Kipindi chake cha ngoma asilia pale Barmedas kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.

Tutakukumbuka daima tulikuoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo haupo nasi. Huu ni wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu kwa mikono yetu miwili.
AMINA!
NAEDWIN SOKO;
MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WANAHABARI JIJINI MWANZA WAMLILIA MAREHEMU MWALIMU SOKORO, ALIEKUWA MHARIRI WA BARMEDAS TV.
WANAHABARI JIJINI MWANZA WAMLILIA MAREHEMU MWALIMU SOKORO, ALIEKUWA MHARIRI WA BARMEDAS TV.
https://2.bp.blogspot.com/-tHrXfqE1rpQ/V4x0lxBJ5dI/AAAAAAAAMqg/uUE8-7vee381rJAe7a_DgLphSndoto3swCLcB/s640/1.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-tHrXfqE1rpQ/V4x0lxBJ5dI/AAAAAAAAMqg/uUE8-7vee381rJAe7a_DgLphSndoto3swCLcB/s72-c/1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/wanahabari-jijini-mwanza-wamlilia.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/wanahabari-jijini-mwanza-wamlilia.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago