Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI USAFI WA MAJI, HALI YA USALAMA BADO SI NZURI

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela akitoa hotuba kwa niaba ya serikali ka...


Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela akitoa hotuba kwa niaba ya serikali katika kongamano hilo. (Picha na Modewjiblog)Katika kuhakikisha kunakuwa na usalama wa maji duniani kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vifo ambavyo vinatokana na uchafu katika maji, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limefanya kongamano la siku moja ambalo limewakutanisha viongozi wa idara za maji za mikoa mbalimbali nchini na kutoka nje ya nchi.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela alisema sehemu kubwa ya vyanzo vya maji zimekuwa vikichafuliwa kutokana na usafi wa binadamu.

Alisema kuwa takwimu zinaonyesha ni asilimia 24 ya watu Afrika ndiyo wanajisaidia katika maeneo ambayo ni salama na idadi iliyobakia wamekuwa wakijisaidia mazingira ambayo yanahatarisha vyanzo vya maji na wengi wao wakijisaidia maporini.

"Kongamano hili linaangalia kuhusu vijidudu vilivyo katika maji ambavyo kwa asilimia kubwa yanachafuka kutokana na usafi ambao anaufanya binadamu na ukiangalia kwa nchi zetu inaonyesha bado uhifadhi wa hizo taka kama kinyesi ambacho baadae huathiri vyanzo vya maji ni mdogo," alisema Lugomela.

Aidha alisema pamoja na maeneo mengine kufanya ujenzi wa vyoo lakini jambo hilo bado sio salama kwa asilimia 100 na hivyo inahitajika kufanyika jitihada za ziada ili kuweza kuviweka vyanzo vya maji katika hali ya usalama.

Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, akielezea umuhimu wa kongamano hilo.

Nae Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, alisema kuwa kongamano hilo lina malengo ya kupata suluhisho ili kuhakikisha watu ambao wanaishi bara la Afrika wanapata maji safi na salama.

Katika ripoti ya mwaka 2014 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO) inaonyesha kuwa watu bilioni 1.8 duniani kote wanatumia maji ambayo yana vijidudu.

Mtaalam wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis akitoa takwamu za usalama wa maji na jinsi taka mwili za binadamu zinavyoyafanya maji yasiwe salama.Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo la siku moja kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI USAFI WA MAJI, HALI YA USALAMA BADO SI NZURI
UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI USAFI WA MAJI, HALI YA USALAMA BADO SI NZURI
https://images-blogger-opensocial.googleusercontent.com/gadgets/proxy?url=http%3A%2F%2Fdewjiblog.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2016%2F07%2FDSC_3944.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/unesco-yakutanisha-wadau-kujadili-usafi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/unesco-yakutanisha-wadau-kujadili-usafi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago