Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI YA MISITU NA WANYAMAPORI YENYE MIGOGORO MBALIMBALI MKOANI TABORA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifany...


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifanya ziara ya kikazi ya siku nne na kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ya Hifadhi ya Misitu na Wanyamapori yenye migogoro. Maeneo hayo ni Hifadhi ya Msitu wa Wembere (Wilaya ya Igunga), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima (Wilaya ya Kaliua), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole (Wilaya ya Skonge),  Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi (Wilaya ya Skonge) na Msitu wa hifadhi wa Ilomero (Wilaya ya Nzega).
 Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani akizungumza na baadhi ya wananchi waliovamia Msitu wa Hifadhi wa Wembere Wilayani Igunga hivi karibuni. Aliwataka wananchi hao kutii sheria za nchi na kusubiri maelekezo ya Serikali ambapo aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kukusanya taarifa mbalimbali zinazohusu hifadhi hiyo na vijiji jirani ambapo zitatumika kumaliza mgogoro huo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa waliovamia Msitu wa Wembere na kuweka makazi, Wilayani Igunga hivi karibuni. Alitoa maelekezo mbali kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania kwa ajili ya kukabili changamoto zilizopo katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga pamoja na viongozi wengine kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA). 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi karibuni. Hifadhi hiyo ambayo imetengwa na vijiji 11 kwa ajili ya kuanzishwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima umevamiwa na wananchi kutoka maeneo ya nje ya vijiji hivyo na kuweka makazi, mifugo na kilimo jambo lililoikwamisha jumuiya hiyo kupewa kibali cha kurasimishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Eng. Makani alitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Kaliua na Halmashauri kutumia mamlaka ya kisheria waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa. 
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua alipotembelea kuona changamoto wa Uhifadhi na kuweka utaratibu wa kuzikabili.
Mmoja wa wananchi waliovamia Hifadhi ya Isawima, Kaliua, Charles Msinda (kulia) akiiomba Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) iwafikirie kuwapa maeneo mbadala baada ya kuondoka katika Hifadhi ya Msitu huo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizungumza na viongozi wa Chama (CCM) na Serikali Wilayani Skonge. Kulia kwake ni mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na jamii wa wavuvi wa Mto Koga, Wilayani Skonge ikiwa na hatua ya kusuluhisha mgogoro kati yao na muwekezaji, Muhsin Abdllah "Shein" ambaye ni Mkurugenzi wa Northern Hunting. Eng. Makani aliwataka viongozi wa Wilaya na Halmashauri kukaa pamoja na muwekezaji huyo na wadau mbaimbali kwa ajili ya kamaliza mgogoro huo. Aliwata viongozi hao kuangaliwa upya vibali vinavyotolewa kwa wavuvi hao ili idadi yake ilingane na ukubwa na mahitaji ya Mto huo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akisikiliza malalamiko kutoka kwa muwekezaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Hunting, Muhsin Abdallah (kushoto)  aliyewekeza katika kitalu cha uwindaji kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole Wilayani Skonge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ipembampazi, Wilayani Skonge Tabora. Wananchi hao wameiomba Serikali iwamegee eneo la hifadhi kwa ajili mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Uluwa, Hifadhi ya Msitu ambao upo chini ya Halmashauri ya Wilaya Kaliua. Eng. Makani alitoa maelekezo mbalimbali kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mkoa ikiwa ni pamoja kuangalia taratibu za kisheria na kimazingira juu ya uwezekano wa ombi hilo na kuliwasilisha Wizarani kwa ajili ya hatua zaidi. (Picha na Hamza Temba - WMU - www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI YA MISITU NA WANYAMAPORI YENYE MIGOGORO MBALIMBALI MKOANI TABORA
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI YA MISITU NA WANYAMAPORI YENYE MIGOGORO MBALIMBALI MKOANI TABORA
https://2.bp.blogspot.com/-_lMWvWi7DjM/V5z46u9VDmI/AAAAAAAAAtg/Kj2xc09PkywDm3D8XLkAhGo0XmJkKNRbQCLcB/s640/DSC_6365.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-_lMWvWi7DjM/V5z46u9VDmI/AAAAAAAAAtg/Kj2xc09PkywDm3D8XLkAhGo0XmJkKNRbQCLcB/s72-c/DSC_6365.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/naibu-waziri-wa-maliasili-eng-ramo_31.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/naibu-waziri-wa-maliasili-eng-ramo_31.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago