Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NDANI YA JIJI LA MWANZA

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya...


  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa. 

Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.
Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya. 
Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara. 
Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba. 
Imetolewa na 
Atley J. Kuni 
Afisa habari na Mahusiano 
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
MWANZA. 
04, Julai, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NDANI YA JIJI LA MWANZA
MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NDANI YA JIJI LA MWANZA
https://4.bp.blogspot.com/-c6vVEbcv6FA/V3p3GwOnOJI/AAAAAAADiQg/b6X_kKh8T1ARZGHHpX2fg_XPN5VNfI7swCKgB/s640/KIAPO%252BMZA..jpg
https://4.bp.blogspot.com/-c6vVEbcv6FA/V3p3GwOnOJI/AAAAAAADiQg/b6X_kKh8T1ARZGHHpX2fg_XPN5VNfI7swCKgB/s72-c/KIAPO%252BMZA..jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/mkuu-wa-mkoa-wa-mwanza-john-mongella.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/mkuu-wa-mkoa-wa-mwanza-john-mongella.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago