Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye suti ya kaki akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick...

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye suti ya kaki akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya .(Picha E.madafa, D.Nyembe)

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.

Ramani ya mradi

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ramani itakayotumika katika mradi huo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza jambo na viongozi wa kisiasa,  kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya mbeya, uongozi wa  kampuni ya Pandahil limited  ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Mwakilishi    wa kampuni ya Pandahil limited  Mbeya Emanuel Kisasi  ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi   eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Eneo ambalo litahusika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla  ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer.
 Mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.
Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjali na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi.
Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali kuu
 Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati
 Hata hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini hayo adhimu ya duniani ya  niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo karibu na maeneo ya gereza hilo la songwe.
 Kwa mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta sanjali na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.Hata hivyo
 Mwisho.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI
MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI
https://2.bp.blogspot.com/-SPWrNA5mKuQ/V3zEXbhDw2I/AAAAAAAAWLs/w85gYsXJRdES7AzsBwWQKqE-_7orZloygCLcB/s640/IMG_6653.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-SPWrNA5mKuQ/V3zEXbhDw2I/AAAAAAAAWLs/w85gYsXJRdES7AzsBwWQKqE-_7orZloygCLcB/s72-c/IMG_6653.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/mkuu-wa-mkoa-wa-mbeya-atembelea.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/mkuu-wa-mkoa-wa-mbeya-atembelea.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago