Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MFALME WA AFRO POP TWENTE PERCENT ARUDI KWENYE GEMU NA SAUTI YA GHARAMA

 Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINE...

 Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
 Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa  na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.

Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.Picha na Sultani Kipingo
---
Na Sultani Kipingo
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki,  huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.

Twenty Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo  za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.

“Nimerudi kuwachinja tena” anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam. “Nimerudi kurudisha sauti ya gharama  kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, ” anaogeza.

Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.

Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses.

“Namkubali sana Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo”, anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na  wasanii nyota kibao wakiwemo  Lady Jay Dee,  Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.

Twenty Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa “Manemane” uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni “Tamaa Mbaya”  na “Ya nini Malumbano” na “Maisha ya Bongo”   

Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. “Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena” alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MFALME WA AFRO POP TWENTE PERCENT ARUDI KWENYE GEMU NA SAUTI YA GHARAMA
MFALME WA AFRO POP TWENTE PERCENT ARUDI KWENYE GEMU NA SAUTI YA GHARAMA
https://3.bp.blogspot.com/-iRBh4qskxOE/V3py7hAPsJI/AAAAAAADiQI/kMGRnHj02FQwykJmvBZq14DRtpSdmgjTQCLcB/s640/11.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-iRBh4qskxOE/V3py7hAPsJI/AAAAAAADiQI/kMGRnHj02FQwykJmvBZq14DRtpSdmgjTQCLcB/s72-c/11.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/mfalme-wa-afro-pop-twente-percent-arudi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/mfalme-wa-afro-pop-twente-percent-arudi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago