Aliyekuwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi, Hafsa Mossi
--- 
 Kumekuwepo na taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa aliyekuwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi, Hafsa Mossi amefariki dunia.
Taarifa kutoka Burundi zinaeleza kuwa serikali ya nchi hiyo tayari imethibitissha kutokea kwa kifo cha mbunge huyo wa EAC na ikielezwa kuwa Hafsa Mossi amekutwa na mauti baada ya kupigwa risasi katika eneo la Buja, Burundi.