Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Su...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri
wa
Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik
aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa
na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri
wa
Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake walioleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa
na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri
wa
Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik
pamoja na ujumbe wake ambao walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo
Salva Kiir kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa
na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
--
Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan Kusini
Rais
wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za serikali ya
Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo.
Ujumbe
huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo
Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.
Waziri
huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama kwa sasa
imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya wanajeshi watiifu
wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar
Akipokea
ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali
ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani
inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi
wa taifa hilo kufanya kazi za maendeleo kwa amani na utulivu.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI zinazohasimiana
kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga
kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo.