Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YANUNUA 620 KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KUZALIWA KWA GS1 NA KUADHIMISHA SIKU YA TWCC

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 ( msibomilia) katika...


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 (msibomilia) katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango la GS1 mara baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange .


 Wanawake kutoka Majukwaa mbali mbali ya Wanawake nchini wakishangilia kwa kujumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wakati maonyesho ya 40 ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati wa kutembelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya jiko lililotengenezwa Tanzania na rafiki wa mazingira  wakati alipotembelea mabanda mabali mbali kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kabati lililotengenezwa kwa mbao ya mnazi wakati alipotembelea moja la banda la wajasiriamali kuotoka Zanzibar wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzana fundi wa kushona nguo mwenye ulemavu wa macho (asiyeona) ambaye anafahamika kama Mtaalamu wa kushona Tanzania Ndugu Abdallah Nyangalio, kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangali moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wanawake wakati wa maonyesho ya kimataifa ya biashara
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ubunifu wa hali ya juu ya gauni la kanga kwenye moja ya mabanda ya wajasiamali wa Kitanzania wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelezo juu ya bidhaa zinazotengenezwa nchini na Bi. Flaviana Tesha wa Kampuni ya Chai Bora wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiuliza maswali mbali mbali alipotembelea banda la Benki ya Watu wa Zanzibar kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
                         .....................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620 Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonyesho ya  40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.
Makamu wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.
Ameleeza kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na  kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Kuhusu uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi  nchini, Makamu wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo chanya na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.

 
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YANUNUA 620 KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KUZALIWA KWA GS1 NA KUADHIMISHA SIKU YA TWCC
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YANUNUA 620 KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KUZALIWA KWA GS1 NA KUADHIMISHA SIKU YA TWCC
https://1.bp.blogspot.com/-AZ9aFnEwZBE/V3gXN0j9SFI/AAAAAAAAxzU/lPLjwPUKUQghkj5f0HgzYoDL5DW-oZQLACLcB/s640/49.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-AZ9aFnEwZBE/V3gXN0j9SFI/AAAAAAAAxzU/lPLjwPUKUQghkj5f0HgzYoDL5DW-oZQLACLcB/s72-c/49.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/makamu-wa-rais-azindua-kampeni-yanunua.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/makamu-wa-rais-azindua-kampeni-yanunua.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago