Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KONGAMANO LA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI MKOANI MWANZA LAFANYA.

Mgeni Rasmi, Meneja wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mkoani Mwanza, Damian John Changa, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa ...


Mgeni Rasmi, Meneja wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mkoani Mwanza, Damian John Changa, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, katika ufungaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza lililohitimishwa jana katika Viwanja vya Gandh Hall Jijini Mwanza. 

Alisema umefika wakati wa vijana kuacha kuilalamikia Serikali huku wakiwa hawajishughulishi katika kujipatia kipato hivyo kongamano hilo anaamini limewafungua vijana wengi mkoani Mwanza ambao watatumia elimu ya ujasiriamali na uwekezaji waliyoipata kutumia fursa zilizopo mkoani Mwanza ili kujikomboa kiuchumi.

Kongamano hilo lilifanyika kwa siku mbili kuanzia jumamosi Julai 16,2016 hadi jana jumapili julai 17,2016 ambapo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania Youth Enterpreurship Organization pamoja na Taasisi ya Vijana Mwanza Saccos kwa lengo la kuwawezesha vijana kukutana pamoja kuzungumza, kujadili na kutathimini kwa pamoja fursa zilizopo mkoani Mwanza na kuzitumia ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni "Kijana ndio Mhimili wa Upaishaji wa Pato la Taifa, Usisubiri kesho, Fursa ni Sasa".
Afisa Maendeleo ya Jamii Jijini Mwanza, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, katika hitimisho la Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza, akizungumza katika hitimisho la kongamano hilo jana.

Alisema kongamano hilo limevunga lengo la kuwafikia vijana 1,100 kwani zaidi ya vijana 2,000 walihudhuria huku pia lengo la kuvifikia vikundi 50 vya wajasiriamali mkoani Mwanza likivukwa baada ya vikundi 150 kujiandikisha na kushiriki katika kongamano hilo.
Beatus Kisusi ambae alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kongamano hilo akizungumza wakati wa ufungaji wake jana.
Florah Magabe ambae alikuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Vijana Wawekezaji na Wajasiriamali mkoani Mwanza, alitanabaisha kwamba lengo ni kongamano hilo kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi ili waweze kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.
Mdau wa Maendeleo Jijini Mwanza ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, akitoa Mada kuhusu "Watu waliopambana na Maisha na kufanikiwa katika harakati za kuzalisha mali".
Mh.Dkt.Antony Diallo ambae ni Mkurugenzi wa Sahara Media Group, akitoa mada juu ya "Ujasiriamali na Uwekezaji katika Mkoa wa Mwanza" katika kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Miongoni mwa watoa Mada katika kongamano hilo ambae alitoa mada juu ya "Umuhimu wa Bima katika Biashara".
Kulwa William Matolwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Kanda ya Ziwa, akitoa mada katika kongamano hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka hilo Kanda ya Ziwa.
George Binagi-GB Pazzo ambae ni blogger wa BMG, akitoa mada juu ya Matumizi akinifu ya Mitandao ya Kijamii na Biashara.
Jummy Peter Masumbuko ambae ni Mratibu Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Ufugaji wa Viumbe Maji kutoka Taasisi ya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi mkoani Mwanza-FETA akitoa mada katika kongamano hilo
Maneno Abubakary kutoka SIDO mkoani Mwanza, akitoa mada katika kongamano hilo.
Donald Kasongi ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Governance Links, akitoa mada katika kongamano hilo.
Mwalimu Beny Mwenda kutoka Chuo cha UKIRIGURU mkoani Mwanza, akitoa mada katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk and Chair Foundation, Sibtain Meghji, akitoa salamu za taasisi hiyo ambayo ilifadhiri kwa asilimia kubwa kongamano hilo ambapo alisisitiza kwamba makongamano ya aina hiyo kufanyika mara kwa mara ili kusaidia kuwapatia vijana elimu ya ujasiriamali na uwekezaji huku akisisitiza zaidi pia fursa za makongamano na maonyesho kama ya Sabasaba pia kufanyika mikoani badala ya kusalia tu Dar es salaam.
Baadhi ya waliohudhuria kongamano hilo akiwemo Mwenyekiti wa Machinga Jijini Mwanza, Masanja Matondo (kushoto), wakifuatilia matukio kwa umakini zaidi
Baadhi ya wadau wakifuatilia Kongamano hilo akiwemo Katibu wa Machinga Jijini Mwanza (kushoto).
Burudani live kutoka kwa Ramyy Ramulla a.k.a Katoto Ka Mama Rama.
Atrey Kuni ambae ni Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliongoza vyema Kongamano hilo.
Wadau katika picha ya pamoja
Mgeni Rasmi (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KONGAMANO LA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI MKOANI MWANZA LAFANYA.
KONGAMANO LA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI MKOANI MWANZA LAFANYA.
https://1.bp.blogspot.com/-fVLFaTgzgMM/V4xZWV1x1wI/AAAAAAAAMpE/nLCotlWYRzoPe1NBjTsqbXSTw8OS_nfXwCLcB/s640/1.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-fVLFaTgzgMM/V4xZWV1x1wI/AAAAAAAAMpE/nLCotlWYRzoPe1NBjTsqbXSTw8OS_nfXwCLcB/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/07/kongamano-la-vijana-wajasiriamali-na.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/07/kongamano-la-vijana-wajasiriamali-na.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago