Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi

Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya ko...Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi.

"Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume - MO Blog)

"Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa kuwapo," alisema Msangi.

Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu wote.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo akitoa neno la ukaribisho katika ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika Bagamoyo, Pwani.

Alisema kupitia kongamano hilo wamekutanisha wataalam wa kodi, wahasibu, walipa kodi, wanasheria, washauri wa kodi na walimu wa kodi kutoka vyuoni ili kuweza kupata maoni ya pamoja na kupata maoni ya makubaliano ya pande zote ambayo yatatumika katika kuendesha chombo hicho.

Na Rabi Hume - MO Blog)
Baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo la siku moja lililofanyika Bagamoyo, Pwani.


Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja (group one).
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja (group two).

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
https://images-blogger-opensocial.googleusercontent.com/gadgets/proxy?url=http%3A%2F%2Fdewjiblog.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2016%2F06%2FDSC_4335.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/tra-yakutanisha-wadau-wa-kodi-kujadili.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/tra-yakutanisha-wadau-wa-kodi-kujadili.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago