Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa ya Uteuzi Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bo...

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia  katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Juni, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa ya Uteuzi Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu
Taarifa ya Uteuzi Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu
https://4.bp.blogspot.com/-zynvQ9vH2xw/V2wMqZ-ulAI/AAAAAAADiHc/68f18hZ5ARAw2KUuju00UtxHJ6dnun7IgCLcB/s640/Rais%252BMagufuli%252Bawasihi%252Bwatanzania%252Bkuungana%252Bna%252Bwaislamu%252Bkuliombea%252Btaifa.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-zynvQ9vH2xw/V2wMqZ-ulAI/AAAAAAADiHc/68f18hZ5ARAw2KUuju00UtxHJ6dnun7IgCLcB/s72-c/Rais%252BMagufuli%252Bawasihi%252Bwatanzania%252Bkuungana%252Bna%252Bwaislamu%252Bkuliombea%252Btaifa.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/taarifa-ya-uteuzi-kutoka-ikulurais-dr.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/taarifa-ya-uteuzi-kutoka-ikulurais-dr.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago