Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

OSHA kuja na mbinu mpya za kuwasaidia wafanyakazi

. Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mwendeshaji wa mafunzo hayo, Andrew Christian ambaye yupo Geneva, Switzerland aliyekuwa ak....

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mwendeshaji wa mafunzo hayo, Andrew Christian ambaye yupo Geneva, Switzerland aliyekuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi.Mwendeshaji wa mafunzo, Andrew Christian akiwa Geneva, Switzerland ambaye alikuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.
--
 
Wakiwa kama wakaguzi wa huduma za afya na usalama kwa wafanyakazi katika maeneo ya kazi, Wakala wa Afya na Usalama sehemu za Kazi (OSHA) wameeleza kuwa wataboresha ukaguzi wao hasa kwa wafanyakazi walio na UKIMWI jinsi wanavyohudumiwa na waajiri wawapo kazini.

Akizungumza na Mo Blog katika mafunzo ya jinsi ya kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa watu walio na UKIMWI, Kaimu meneja usajili na takwimu za afya na Usalama OSHA, Dk. Abdalssalaam Omary, alisema kupitia mafunzo hayo wanataraji kuboresha ukaguzi zao ambazo zifanywa katika maeneo ya kazi ambazo zinakuwa zinawahusu watu walio na UKIMWI.

“Tunaamini kuwa baada ya mafunzo tutakuwa na maboresho katika kaguzi zetu sababu tumepata nafasi ya kukutana na wenzetu kutoka sehemu nyingine na kubadilishana uelewa kwahiyo tutakuwa tofauti na awali,” alisema Dk. Omary.

Alisema pamoja na kujipanga kuboresha kaguzi zao alisema kuwa bado wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa muda mwingine zinaweza kuwa zinawafanya wakwame na kueleza changamoto hizo ni pamoja na fedha na madaktari kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wafanyakazi.

Kwa upande wa serikali kupitia Kaimu Kamishna wa Kazi Msaidizi, Rehema Moyo alisema kuna sheria ambazo zimewekwa ambazo zinakataza waajiri kufanya vitendo vya ubaguzi kwa wafanyakazi na hivyo kama kuna waajiri wanawafanyia vitendo ambavyo havikubaliki kisheria basi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakani kujibu mashitaka yanayowakabili.

“Sera zipo utekelezaji ndiyo mgumu kuna vitendo vya ubaguzi lakini kujua ndiyo inakuwa changamoto maana ni mpaka muhusika aseme na sheria zipo kama mwajiriwa akikutwa na hatia anaweza hata kufungwa gerezani au kupigwa faini,” alisema Bi. Moyo.

Nae Mratibu wa maswala yanayohusiana na UKIMWI maeneo ya kazi kutoka Shirika la Kazi (ILO), Getrude Sima, alisema kupitia mafunzo hayo wanaamini washiriki wataweza kupata kitu kipya ambacho kitawasaidia katika kaguzi wanazozifanya ili waweze kutambua zaidi matatizo yanayowakuta wagonjwa wa UKIMWI wawapo kazini na jinsi ya kuwasaidia

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: OSHA kuja na mbinu mpya za kuwasaidia wafanyakazi
OSHA kuja na mbinu mpya za kuwasaidia wafanyakazi
https://images-blogger-opensocial.googleusercontent.com/gadgets/proxy?url=http%3A%2F%2Fdewjiblog.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2016%2F06%2FDSC_0266.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/osha-kuja-na-mbinu-mpya-za-kuwasaidia.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/osha-kuja-na-mbinu-mpya-za-kuwasaidia.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago