Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MGAHAWA WA KIPEKEE WA PWEZA WAZINDULIWA JIJINI DAR

Mgahawa huu waleta mapishi mapya ya makange ya pweza, kamba (prawns) na ngisi. Samaki aina ya pweza amekuwa maarufu sana hapa nchini ...


Mgahawa huu waleta mapishi mapya ya makange ya pweza, kamba (prawns) na ngisi.

Samaki aina ya pweza amekuwa maarufu sana hapa nchini Tanzania, kutokana na ladha yake tamu na faida zake kiafya. Kutokana na umaarufu huo vijana wa kitanzania wameamua kuwa wabunifu zaidi na kuanzisha mgahawa wa kisasa maalum kwa ajili ya mapishi ya pweza, kamba (prawns) na ngisi unaoitwa Pweza Cafe.

Akiongea na mwanidishi wetu, mmoja wa wamiliki wa mgahawa huo bwana Alfred Kiwuyo alisema, "Sisi wenyewe ni wapenzi wa supu na nyama ya pweza, kamba (prawns) na ngisi lakini mazingira ya awali ya kuuza vyakula hivi kwenye vituo vya daladala na makutano ya barabara kadhaa hapa jijini yalikuwa yanatukatisha tamaa hasa ukizingatia usafi na mapishi yenyewe haukuwa wa kuridhisha sana. Sasa tukajiuliza swali je, haiwezekani kuwa na sehemu ya kisasa zaidi ya kuuza pweza, ngisi na kamba (prawns) na kukawa na mapishi zaidi ya haya. Ndipo tukaamua kuanzisha mgahawa huu ambapo tunapika mpaka makange ya pweza, prawns (kamba) na ngisi."

Muonekano wa Pweza Cafe kwa nje.

Vivyo hivyo akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wateja waliofika kwenye mgahawa huo wa kipekee nchini alisema, "Mimi nimekula makange ya pweza na ni mara yangu ya kwanza na nimeyapenda kwa kweli, ni matamu. Kwa mara ya kwanza nilivyosikia makange ya pweza nilishtuka kwanza nikasema lazima niyaonje kwa kuwa tumezoea kula makange ya kuku,ng'ombe, na mbuzi lakini sijawahi kuonja makange ya pweza."

Watafiti wa masuala ya kiafya wanasema, gramu 100 za nyama ya pweza ina madini na vitamini za kutosha kwa mahitaji ya mwili wa binadamu kwa siku. Kwa mfano kiwango hiki cha nyama ya pweza kinampatia mwanadamu mahitaji yake ya siku ya madini ya chuma, seleniamu na vitamini B-12. Madini haya na Vitamini hizi ni muhimu katika kuusaidia mwili kupambana na magonjwa,kutengeneza seli hai nyekundu za damu na kuhakikisha ubongo unafanya kazi yake vizuri.

Makange ya Prawns yakiwa tayari kwa ajili ya mteja Pweza Cafe.

Kuanzishwa kwa Pweza Cafe iliyopo nyuma ya jengo la tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia, Kijitonyama ni mfano wa kuigwa kwa vijana wabunifu na wenye ndoto za kuwa wajasiriamali nchini hivyo basi ni muhimu kwa vijana wengine kuangalia ni biashara zipi zinaweza kuboreshwa katika jamii yetu na kutengeneza ajira kwa vijana wengine zaidi.

Unaweza kufuatilia zaidi kuhusu mgahawa huu kwa kutembelea tovuti yao: https://www.instagram.com/pwezacafe/

Rosti ya prawns inayopatikana Pweza Cafe.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MGAHAWA WA KIPEKEE WA PWEZA WAZINDULIWA JIJINI DAR
MGAHAWA WA KIPEKEE WA PWEZA WAZINDULIWA JIJINI DAR
https://images-blogger-opensocial.googleusercontent.com/gadgets/proxy?url=http%3A%2F%2Fdewjiblog.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2016%2F06%2FPweza-Cafe.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/mgahawa-wa-kipekee-wa-pweza-wazinduliwa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/mgahawa-wa-kipekee-wa-pweza-wazinduliwa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago