Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI AFUTURU NA WATOTO YATIMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na ...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.


 Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
 Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba  wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima  iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.

---

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea watoto yatima nchini na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha wamiliki na  vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha Mboni Show  hafla iliyojumuisha watoto yatima 283 kutoka Vituo vitano vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea watoto yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watoto hao na sio vinginevyo.
Kuhusu malezi ya Watoto yatima, Makamu wa Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu bora,upendo na si kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali.
Aidha, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba jamii kuweka mipango mizuri ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto yatima kwa kuwa nao wana haki ya kuishi vizuri kama watoto wengine.
 


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI AFUTURU NA WATOTO YATIMA
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI AFUTURU NA WATOTO YATIMA
https://4.bp.blogspot.com/-S-phHZBgm8U/V3ToMR2keXI/AAAAAAAAxxM/zADzTVZhFcM70h2XoOq_gM6FQoEAJjJ-ACLcB/s640/38.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-S-phHZBgm8U/V3ToMR2keXI/AAAAAAAAxxM/zADzTVZhFcM70h2XoOq_gM6FQoEAJjJ-ACLcB/s72-c/38.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassani.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassani.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago