Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI FUTARI YA WATOTO JUNI 26

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la futari maa...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la futari maalum iliyoandaliwa kwa watoto waishio Mazingira magumu na hatarishi tukio litakalofanyika Juni 26.2016 ndani ya viwanja vya shule ya Sekondari ya Wavulana ya Azania, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Juni 21.2016, Mkurugenzi wa kampuni ya Nisha’s Film Production, Bi. Salma Jabu “Nisha” ameeleza kuwa, tayari maandalizi yote yamekamilika na tukio hilo maalum litafanyika katika viwanja hivyo vya shule ya Azania ambapo Makamu huyo wa Rais pamoja na viongozi wengine watahudhuria pia wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mbunge wa Ilala, Idd Hassan Zungu pamoja na viongozi wa dini na wageni wengine waalikwa.
Akielezea suala hilo, Nisha amebainisha kuwa, akiwa kama msanii na ambaye ni kioo cha jamii na pia ni balozi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu cha New Hope Family kilichopo Kibada Mwasonga-Dar es Salaam, hivyo kwa tukio hilo ni moja ya kurudisha fadhira kwa jamii pamoja na kuweza kukutana nao kwa pamoja.
“Wito kwa dini yetu ya kiislamu hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu tunapaswa kutoa Dhaka pamoja na kuonyesha upendo kwa wenzetu wanaoishi katika mazingira magumu hasa watoto Yatima, Walemavu, wanaoishi mitaani pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi kwa kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali ambazo zinaweza kuwa sehemu ya faraja kwao” alieleza Nisha.
Futari hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Juni 26.2016 katika uwanja huo wa shule ya sekondari Azania ambapo tiukio hilo linatarajia kuanza majira ra saa 10 jioni na litaendelea hadi saa mbili usiku.
Watoto na watu wote waishio pembezoni mwa jiji la Dar e Salaam wanatarajiwa kufikiwa ambapo pia viongozi na wasimamizi wa vituo vilivyopo Jijini Dar es Salaam wameombwa kufahamishwa tukio hilo kwa ushiriki wao ambapo pia wanaweza kuwasiliana kupitia namba 0676894246 ama 0789586057.
Aidha, Nisha akijibu swali la mwanahabari wa mtandao huu juu ya kama yupo tayari kutengeneza filamu inayoelezea watoto waishio katika mazingira magumu, ambapo ameeleza kuwa tayari amesha andaa filamu hiyo na ndani ya miezi miwili hadi mitatu inatarajia kuingia sokoni.
“Kwa sasa tayari nimesha andaa filamu inayozungumzia mazingira ya watoto waishio mazingira magumu na pia ndani ya filamu hii, Msanii Joti ameweza kushiriki pia” alijibu Nisha.
Aidha, baadhi ya filamu zake ni pamoja na Mtaa kwa Mtaa, Macho yangu, Kashfa, Gumzo, Zena na Betina na zingine nyingi.
Tazama MO tv, hapa kuona tukio hilo:
DSC_7923Meneja wa Nisha Film Production, Bwana Myovela Mfuasi akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo la kampuni yao hiyo juu ya kufuturisha watoto waishio katika mazingira magumu itakalofanyika Juni 26.2016 katika shule ya sekondari ya Azania.
DSC_7942Afisa Habari wa kampuni ya Nisha Film Production, Baraka Nyaganda, wa pili kutoka kushoto, akizungumza katika tukio hilo anayemfuatia ni Meneja wa kampuni hiyo, Bi. Salma Jabu 'Nisha' na wa kwanza kulia ni mmoja wa watoto wanaopatiwa misaada, Mtoto Lazaki Rashid.
DSC_7921Mkurugenzi wa kampuni ya Nisha Film Production, Bi. Salma Jabu 'Nisha' akipitia taarifa hiyo kwa wanahabari
DSC_7929Mkutano huo ukiendelea..
DSC_7933Mkurugenzi wa kampuni ya Nisha Film Production, Bi. Salma Jabu 'Nisha' akisoma taarifa hiyo kwa wanahabari (Hawapo pichani).
DSC_7926Mkurugenzi wa kampuni ya Nisha Film Production, Bi. Salma Jabu 'Nisha' akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI FUTARI YA WATOTO JUNI 26
MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI FUTARI YA WATOTO JUNI 26
https://i.ytimg.com/vi/R-N50iI_tQ8/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/R-N50iI_tQ8/default.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/makamu-wa-rais-mama-samia-mgeni-rasmi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/makamu-wa-rais-mama-samia-mgeni-rasmi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago