Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wa...



Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akifafanua jambo ndani ya duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani

Baadhi ya bidhaa zinavyoonekana ndani ya duka hilo.





Sehemu ya mchele na bidhaa zingine za nafaka zinazopatikana katika duka hilo.


Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za matunda yanayopatikana dukani hapo.



Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya maboga bidhaa zinazopatikana dukani hapo.

Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha mboga mboga za aina mbalimbali zinazopatikana dukani hapo.



Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za asali dukani hapo.











---
Kampuni
ya Tomoni Farms Limited, inayomilikiwa na wazawa, wakijishughulisha na
Kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya Matunda na Mbogamboga, wamefungua
duka na Mgahawa wa Kisasa kwa ajili ya uuzaji wa mazao yao katika hali
ya usafi na usalama wa hali ya juu uliopo eneo la jirani na Victoria,
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar Es Salaam,
wakati wa utambulisho wa duka hilo na shughuli zinazofanywa na kampuni
hiyo ya Tomoni Farms Limited, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni hiyo
Bwana Franklin Bagalla ameeleza kuwa, wameamua kuwasogezea watanzania
bidhaa bora za kilimo ambazo watazipata moja kwa moja kupitia duka lao
hilo na watajiona kama wapo shambani ama bustanini kwa namna ya
uwekezaji wao walivyoweza kuuandaa ikiwemo mazingira safi na utunzaji wa
kisasa kutoka shambani hadi kumfikia mlaji.
“Baada
ya kuwekeza kwa miaka mine katika kilimo cha Matunda na Mboga mboga kwa
kutumia teknolojia ya umwagiliaji, huku tukiwa na uhakika wa kutoa
mazao Mwaka mzima, sasa tumewekeza katika miundo mbinu ya kuhakikisha
mazao yetu yanawafikia walaji yakiwa katika hali ya usafi na usalama.
Hivyo kupitia katika duka letu hili la kisasa hapa Dar es Salaam linatoa
fursa kwa wananchi kujipatia bidhaa za kila aina na watazipata kwa hali
ile ile kama zipo shambani na tunawakaribisha sana” alieleza Bwana
Bagalla.
Aliongeza
kuwa, Mazao yote yanavunwa na kusafirishwa katika magari maalumu
kutegemea na uhitaji wa mazao hayo, na hupokelewa, kuchambuliwa na
hatimaye kuhifadhiwa katika jokofu kubwa la baridi kuhakikisha kwamba
ubora wa bidhaa unabakia kama ule wa shambani na baada ya hapo bidhaa
hizo huuzwa kupitia duka hilo la kisasa na zingine hutumika katika
mgahawa wao ambao pia unatengeneza aina mbali mbali za Juice nzito na
nyepesi ambazo mara nyingi wataalam wa Afya wanashauri watu kutumia.
Kwa
upande wake, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Bwana
Willybroad Alphonce amesema kuwa katika kufikia malengo na uendeshaji
wameweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha cha Zaidi ya Bilioni moja.
Na
kuongeza kuwa, wakiwa miongoni mwa Watanzania wazawa, wamewaomba
watanzania kuwaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia
mkulima aliyoko kijijini ambaye bidhaa zake zinaharibika huku mijini
zikihitajika kwa wingi, kwani licha ya wao kuendesha shughuli za kilimo
pia wamekuwa wakinunua baadhi ya mazai kutoka kwa wakulima wengine
ikiwa tu na lengo la kusaidia soko hasa la ndani.
“
Wateja watakao fika dukani kwetu watajipatia vitu mbalimbali. Ni wakati
muafaka sasa kuchangamkia fursa hii ya bidhaa za mashambani ambazo
zinatoka kwenye ardhi yetu ya nyumbani yenye rutuba za kutosha na
uhifadhi wa hali ya usafi na usalama kwa mlaji.
Tunawakaribisha
wote wanaotambua umuhimu wa kupata lishe bora kupitia matunda na mboga
mboga huku tukiwasisitiza wale wote wenye watoto kuhakikisha wanawaleta
pale Farm Fresh Bar waanze kuzoea toka mapema kuchangamana katika Bar
zenye manufaa Kiafya” alimalizia
Tomoni
Farms Limited inaendesha duka hilo la kisasa la mazao ya shambani, pia
ina mgahawa na Bar maalum ambayo inahudumia bidhaa za matunda pekee
ikiwemo juice za kila aina pamoja na masuala yote ya vyakula vya mboga
mboga ambavyo ni vya asili.