Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya shilingi elfu hamsini.

Mkurugenzzi wa Uuguzi Hospital ya Taifa Muhimbili Bibi. Agness Mtawa wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Ku...

Mkurugenzzi wa Uuguzi Hospital ya Taifa Muhimbili Bibi. Agness Mtawa wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitenggo cha Mawasilinano Bw. Aminiel Aligaesha.

 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),  Bw. Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.


 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo hicho LEO katika hospitali hiyo.
---

Na: Frank Shija, MAELEZO
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya shilingi elfu hamsini.

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

Aligaesha amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kutoa fursa kwa Hospitali hiyo kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

Aliongeza kuwa kutokana na kutolewa kwa huduma ya chakula hospitalini hapo kutasababisha mabadiliko ya  ratiba ya kuona wagonjwa kwa kuondoa muda wa saa 6 – 8 mchana ambao ulikuwa unatumiwa na ndugu kwa kuleta chakula kwa wagonjwa wao, badala yake muda wa kuona wagonjwa utabaki saa 12.00 -1.00 Asubuhi na saa 10.00 -12 jioni.

Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa anaweza kutumia kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri.

Kwa uande wake Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali hiyo Agness Mtawa amesema kuwa huduma hizo za chakula zitaondoa adha kwa ndugu wa wagonjwa kwa ambao walikuwa wanatumia muda huo kufika Hospitalini hapo.

Agness iliongeza katika huduma hiyo ya chakula wahudumu na wauguzi ndiyo wenye jukumu la kusaidia wagonjwa wenye mahitaji maalumu kama ktutoweza kujilisha wenyewe.

Huduma hiyo ya chakula itatolewa kupitia mzabuni aliyepatikana na kuongeza kuwa mgonjwa atachangia gharama ya shilingi 50,000 ambapo shilingi 10,000 itatumika kwa huduma ya Kitanda, huduma ya ushauri wa Daktari 10,000 na shilingi 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku muda wa siku tano.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya shilingi elfu hamsini.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 1 mwezi Julai 2016 ambapo mgonjwa atachangia gharama ya shilingi elfu hamsini.
https://2.bp.blogspot.com/-AMYRwxR_t1M/V2lLr2nWoJI/AAAAAAADh_M/xmz79b6Mbw4_slPX8VbrRTRcBkLE7u2cwCLcB/s640/mul31.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-AMYRwxR_t1M/V2lLr2nWoJI/AAAAAAADh_M/xmz79b6Mbw4_slPX8VbrRTRcBkLE7u2cwCLcB/s72-c/mul31.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/hospitali-ya-taifa-ya-muhimbili-kuanza.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/hospitali-ya-taifa-ya-muhimbili-kuanza.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago