Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiw...


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. --- Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa hapo jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la upatikanaji wa madawati, ambao kikomo chake ni mwisho wa mwezi huu. Mashindano haya ya fainali za Copa-UMISSETA yalilenga kuzikutanisha timu za mikoa mbalimbali nchini kwa pamoja Jijini Mwanza, zikiwa zimeundwa na wachezaji mbalimbali kutoka shule za sekondari ili wachuane kwenye michezo na sanaa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. --- “Thamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI iko pale pale, tukiwa tumejidhatiti kuendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha Nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi. Tutaendelea kuunga mkono na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana,” alisema David Karamagi, Mwakilishi Mkazi wa Coca-Cola Tanzania. 

Karamagi aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola Tanzania inayo imani ya dhati na ikiamini ya kwamba mashindano ya michezo yanayoanzia ngazi ya chini kabisa ndiyo namna thabiti nay a kipekee katika kuibua vipaji vya wachezaji nchini. Pia Karamagi alisema kuwa, wakati wadau wakisubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe mpya za kurejewa kwa fainali za mashindano haya nchini, Coca-Cola Tanzania ilishajipanga kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu za mikoa inayoshiriki. Hivyo basi, kwa udhamini ulioingiwa mwaka huu, Coca-Cola Tanzania itaweza kupanua wigo wa ushirikishwaji wa michezo murua zaidi mbali ya mpira wa miguu, hasa kwa kuweza kujumuisha mpira wa kikapu. “Kampuni ya Coca-Cola nchini tutaendelea na dhamira yetu ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbali mbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na UMISSETA na Copa Coca-Cola’” alimalizia Karamagi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA
COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA
https://3.bp.blogspot.com/-m1DHCZB8Dug/V2Eb182NpzI/AAAAAAABuZE/HAMMMF9dT183FjrEN-i8zTOW3cZi6djIwCLcB/s640/IMGL0838.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-m1DHCZB8Dug/V2Eb182NpzI/AAAAAAABuZE/HAMMMF9dT183FjrEN-i8zTOW3cZi6djIwCLcB/s72-c/IMGL0838.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/06/coca-cola-kuendelea-kudhamini.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/06/coca-cola-kuendelea-kudhamini.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago