Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa ...


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Mhe. Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa waadilifu, kufanyanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa na  kuifanya Tanzania kuendelea kupaa katika medani za kimataifa.
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi ya mkutano kwa Mhe. Waziri, Viongozi wa TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo  kumkaribisha Mhe. Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba    
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika utendaji wa kazi.
Mjumbe kutoka TUGHE-Taifa, Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa taarifa ya wafanyakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo
Afisa Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga
Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri na Wafanyakazi bora wa Idara zote za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
https://1.bp.blogspot.com/-6C35SP0L2Jo/V0gbklrAynI/AAAAAAAAoZk/Db8PlS04bT0mOcbJsDUcKM-5GxvcNOJBQCLcB/s640/719A0076.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-6C35SP0L2Jo/V0gbklrAynI/AAAAAAAAoZk/Db8PlS04bT0mOcbJsDUcKM-5GxvcNOJBQCLcB/s72-c/719A0076.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/waziri-mahiga-afungua-mkutano-wa-baraza.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/waziri-mahiga-afungua-mkutano-wa-baraza.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago